Maelfu ya raia wa Sudan Kusini wakimbilia Sudan
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i26320-maelfu_ya_raia_wa_sudan_kusini_wakimbilia_sudan
Maelfu ya raia wa Sudan Kusini wamekimbilia Sudan kutokana na matatizo mengi yanayoikabili nchi yao ukiwemo ukame.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 13, 2017 03:28 UTC
  • Maelfu ya raia wa Sudan Kusini wakimbilia Sudan

Maelfu ya raia wa Sudan Kusini wamekimbilia Sudan kutokana na matatizo mengi yanayoikabili nchi yao ukiwemo ukame.

Mtandao wa habari wa al Yaum al Sabí umeripoti habari hiyo na kunukuu taarifa ya ubalozi wa Sudan Kusini mjini Khartoum ukisema kuwa, takwimu za awali zinaonesha kwamba karibu watu 35 elfu wameingia nchini Sudan kutokea Sudan Kusini kwa sababu ya ukame.

Ubalozi huo umesema, msafara wa misaada ya chakula umetumwa Sudan Kusini kwa ajili ya kuwasaidia wakimbizi wanaokabiliwa na hali mbaya ya ukame.

Machafuko na uasi umeiletea hasara kubwa nchi changa ya Sudan Kusini

 

Kitengo cha takwimu cha Sudan Kusini kwa mara ya kwanza kimekiri kuwa vita vya ndani vya miaka mitatu sasa nchini humo vimepelekea kuzuka ukame mkubwa katika baadhi ya maeneo ya jimbo la Unity.

Karibu nusu ya wananchi wa Sudan Kusini wanahitajia misaada ya dharura ya chakula na madawa, na wanaishi katika ukosefu mkubwa wa usalama.