Makumi wauawa katika mashambulizi ya waasi CAR
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i26844-makumi_wauawa_katika_mashambulizi_ya_waasi_car
Zaidi ya watu 50 wameuawa katika mashambulizi yanayofanywa maasi wanaobeba silaha huko Jamhuri ya Afrika ya Kati.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Mar 25, 2017 11:55 UTC
  • Makumi wauawa katika mashambulizi ya waasi CAR

Zaidi ya watu 50 wameuawa katika mashambulizi yanayofanywa maasi wanaobeba silaha huko Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Ripoti zinasema kuwa, mashambulizi ya waasi hao yaliyoanza Jumanne iliyopita hadi sasa katika kijiji kimoja cha katikati mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati yameua watu wasiopungua 59 na kujeruhi makumi ya wengine. 

Wakazi wa vijiji vya Agoudou Manga, Yasseneme na Ngouyanza wanasema mashambulizi hayo yanafanywa na waasi wa kundi la Seleka eti kwa shabaha ya kulipiza kisasi dhidi ya wakazi wa vijiji hivyo. 

Hivi karibuni Umoja wa Mataifa na taasisi nyingine za kimataifa zilieleza wasiwasi wao kuhusu kushadidi mgogoro wa kibinadamu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na kusema kuwa zinakabiliwa na matatizo katika kufikisha misaada kwa waathirika katika nchi hiyo. Taarifa zinasema nusu ya jamii ya watu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wanahitaji misaada ya kibinadamu. 

Hali ya usalama CAR inatia wasiwasi mkubwa

Nchi hiyo ilitumbukia katika machafuko na vita vya ndani mwaka 2013 baada ya kuibuka mapigano ya kikabila na kupinduliwa serikali iliyokuwepo madarakani. Mapigano hayo yalisababisha ukosefu mkubwa wa amani na kuwalazimisha maelfu ya raia wa nchi hiyo kuwa wakimbizi ndani ya nchi na katika nchi jirani.