Afrika Kusini yakanusha kutumba jeshi Nigeria kupambana na Boko Haram
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i2758-afrika_kusini_yakanusha_kutumba_jeshi_nigeria_kupambana_na_boko_haram
Jeshi la Afrika Kusini limekanusha habari kuwa litatatuma askari nchini Nigeria kupambana na wapiganaji wa kundi la Boko Haram.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 09, 2016 23:12 UTC
  • Afrika Kusini yakanusha kutumba jeshi Nigeria kupambana na Boko Haram

Jeshi la Afrika Kusini limekanusha habari kuwa litatatuma askari nchini Nigeria kupambana na wapiganaji wa kundi la Boko Haram.

Msemaji wa jeshi hilo Bw Siphiwe Dhlamini amesema hakuna uamuzi uliofikiwa kuhusu kutuma wanajeshi kupambana na kundi la hilo.

Bw Siphiwe amelazimika kukanusha habari hiyo kutokana na uvumi ulioenea kwenye vyombo vya habari, kuwa moja kati ya mambo ambayo Rais Zuma alifanya kwenye ziara yake ya siku mbili nchini Nigeria iliyomalizika siku ya Jumatano, ni kukamilisha mazungumzo kuhusu kutuma kikosi maalum cha jeshi la Afrika Kusini kupambana na kundi la Boko Haram. Uvumi huo ulienea zaidi baada ya mawaziri wa ulinzi wa nchi hizo mbili kukutana.

Hata hivyo taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya Rais Jacob Zuma na Rais Muhamadu Buhari kukutana , ilisisitiza haja ya ushirikiano wa kikanda na juhudi za bara zima la Afrika kupambana na ugaidi na makundi yenye misimamo mikali.