Mripuko wajeruhi watu wawili mjini Mogadishu, Somalia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i28416-mripuko_wajeruhi_watu_wawili_mjini_mogadishu_somalia
Duru za usalama nchini Somalia zimetangaza habari ya kutokea mripuko wa bomu mjini Mogadishu Somalia na kujeruhi watu wawili.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 29, 2017 11:01 UTC
  • Mripuko wajeruhi watu wawili mjini Mogadishu, Somalia

Duru za usalama nchini Somalia zimetangaza habari ya kutokea mripuko wa bomu mjini Mogadishu Somalia na kujeruhi watu wawili.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, mripuko huo umetokea karibu na gari ya mbunge mmoja wa Somalia.

Hadi tunapokea habari hii kulikuwa hakujatolea idadi hasa ya hasara iliyosababishwa na mripuko huo na hakuna kundi lolote lililotangaza kuhusika, ingawa kundi la al Shabab ndilo lenye historia ya kufanya mashambulizi ya namna hiyo huko Somalia.

Wakati huo huo Yusuf Jamal, Meya wa Mogadishu amesema, hali ya kiusalama katika mji mkuu huo wa Somalia imekuwa nzuri hivi sasa ikilinganishwa na huko nyuma ingawa pia amesema kuna udharura wa kuendelezwa mapambano dhidi ya ugaidi hususan vitisho vya kiusalama vinavyosababishwa na kundi la al Shabab.

Raia akiangalia athari zilizosababishwa na mripuko wa bomu mjini Mogadishu

 

Umoja wa Afrika umetuma kikosi chake katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika. Kikosi hicho cha AMISOM kina wanajeshi kutoka Uganda, Kenya, Burundi na Ethiopia pamoja na polisi kutoka Nigeria na Sierra Leone. Askari zaidi ya 22 elfu wanaunda kikosi hicho cha AU kwa ajili ya kupambana na kundi la al Shabab huko Somalia.

Ingawa kundi la al Shabab limefurushwa katika miji yote mikubwa na maeneo muhimu ya Somalia, lakini bado lina wanamgambo wake katika baadhi ya vijiji na miji na linafanya mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya raia na maafisa wa Serikali.