Idadi ya Waislamu nchini Madagascar imeongezeka ndani ya miaka saba iliyopita
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i30036-idadi_ya_waislamu_nchini_madagascar_imeongezeka_ndani_ya_miaka_saba_iliyopita
Jamii ya Waislamu nchini Madagascar imeongezeka zaidi katika kipindi cha miaka saba ya hivi karibuni.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 04, 2017 10:48 UTC
  • Idadi ya Waislamu nchini Madagascar imeongezeka ndani ya miaka saba iliyopita

Jamii ya Waislamu nchini Madagascar imeongezeka zaidi katika kipindi cha miaka saba ya hivi karibuni.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa hivi karibuni, idadi ya Waislamu nchini Madagascar imeongezeka katika kipindi cha miaka saba kutoka asilimia 10 na kufikia asilimia 15. Jean Jack Ravana, amesema kuwa sababu ya ongezeko hilo la wafuasi wa dini ya Uislamu nchini humo, ni kwamba mbali na pande za kimaanawi, dini ya Uislamu inajumuisha pia pande muhimu za kijamii,

Moja ya vituo vya Kiislamu nchini Madagascar

kiasi kwamba muundo wa namna ya maisha ya mtu binafsi na jamii ya Waislamu umekuwa ukihusika katika kuwavutia watu wa dini nyingine kujiunga na Uislamu. Akizungumzia kuwa dini ya Kiislamu haina mafungamano yoyote na harakati za makundi ya kigaidi yanayotekeleza jinai na mauaji, Ravana amesema kuwa, Uislamu unapinga kila aina ya mauaji ya kuvizia, kujiripua na ukatili wowote na kinyume chake dini hiyo inasisitizia kuishi na watu wengine kwa amani na udugu, kama ambavyo pia inawalingania watu wa dini nyingine kuingia katika Uislamu kwa amani pasi na utumiaji mabavu.

Bendera ya Madagascar