Misri yawekwa katika orodha nyeusi ya ILO
Shirika la Kazi Duniani (ILO) limeiweka Misri kwenye orodha nyeusi kwa mara ya nne.
Orodha hiyo inakusanya majina ya nchi zinazokiuka haki za wafanyakazi na zisizotekeleza majukumu yao kuhusu sheria za shirika hilo.
Kabla ya hapo jina ya Misri lilikuwa limewekwa kwenye orodha hiyo mara tatu. Orodha nyeusi ya sasa ya Shirika la Kazi Duniani ina majina ya nchi 25 zinazokiuka haki za wafanyakazi. Nchi nyingine za Afrika zinazoonekana kwenye orodha hiyo ni Sudan, Mauritania, Algeria na Libya.
Mratibu wa Kituo cha Huduma cha Jumuiya ya Wafanyakazi nchini Misri, Kamal Abbas amesema sababu ya kuwekwa jina la Misri katika orodha hiyo ya ILO ni mienendo ya kikatili ya serikali ya Cairo dhidi ya wafanyakazi.