Jul 09, 2017 14:02 UTC
  • Hali ya haki za binadamu Sudan yazidi kukosolewa

Duru mbalimbali zinaripoti kuwa, faili la hali ya haki za binadamu na uhuru nchini Sudan limezusha utata mkubwa, na kwamba serikali ya nchi hiyo sasa inaandamwa vikali na jumuiya za kiraia na kimataifa.

Gazeti la al Qudsul Arabi linalochapishwa katika nchi kadhaa limeripoti kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Sudan kwamba, kwa sasa nchi hiyo inaandamwa vikali na mashinikizo ya kimataifa na kwamba Sudan ambayo iliwekwa kwenye orodha ya nchi zinazokiuka haki za binadamu tangu mwaka 2015, inakabiliwa na matatizo mengi.

Wanaharakati wanatiwa ndani ovyo nchini Sudan

Ripoti hiyo imesema kuwa, kuswekwa jela wanaharakati wa masuala ya kisiasa, kufungwa magazeti, kuharibiwa makanisa na kubanwa uhuru wa watu buinafsi nchini Sudan ni miongoni mwa mambo yanayoitia wasiwasi mkubwa jamii na taasisi za kimataifa.

Kufuatia hali hiyo, Umoja wa Ulaya umeitaka serikali ya Khartoum kufanya jithada za kuboresha hali ya haki za binadamu na kutangaza kwamba, unafuatilia suala hilo kwa makini. 

 

Tags