Muuaji wa watalii wa kigeni Misri atiwa nguvuni
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i31786-muuaji_wa_watalii_wa_kigeni_misri_atiwa_nguvuni
Mtu aliyehusika na mauaji ya watalii wawili wa kigeni kwa kutumia silaha baridi amekamatwa na vyombo vya usalama nchini Misri.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 15, 2017 01:10 UTC
  • Muuaji wa watalii wa kigeni Misri atiwa nguvuni

Mtu aliyehusika na mauaji ya watalii wawili wa kigeni kwa kutumia silaha baridi amekamatwa na vyombo vya usalama nchini Misri.

Ripoti zinasema kuwa, muuaji huyo aliogelea na kufika katika Hoteli ya Hurghada iliyoko pwani na kuwashambulia watalii wa kigeni kwa kutumia silaha baridi. 

Vyombo vya usalama vya Misri vimetangaza kuwa, watalii wawili wa kike kutoka Ujerumani wameuawa katika shambulizi hilo. Awali ilitangazwa kuwa watalii waliouawa ni raia wa Ukraine. Watalii wengine wanne kutoka Jamhuri ya Czech na Armenia wamejeheruhiwa katika hujuma hiyo. 

Hadi sasa sababu ya hujuma hiyo bado haijajulikana na vyombo vya usalama vya Misri vinaendela kufanya uchunguzi.