Sep 13, 2017 02:33 UTC
  • Nigeria yaanza kuchunguza ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanywa na jeshi

Tume iliyoundwa na serikali ya Nigeria imeanza kuchunguza ukikwaji wa haki za binadamu uliofanywa na jeshi la nchi hiyo.

Tume hiyo inachunguza madai yaliyowasilishwa na makundi mbalimbali ya kutetea haki za binadamu ya ndani na nje ya Nigeria likiwemo lile la Amnesty International ambayo yanasema jeshi la Nigeria linakiuka haki za binadamu katika kile kinachosemekana ni mapambano dhidi ya waasi.

Tume hiyo iliyoundwa na Rais wa Nigeria imeahidi kwamba itachunguza madai hayo ya ukiukwaji wa haki za binadamu kwa mujibu wa Mkabaka Geneva na hati ya Umoja wa Afrika kuhusu haki za binadamu na Katiba ya Nigeria. 

Hata hivyo makundi mbalimbali ya Nigeria yanatilia shaka kwamba tume hiyo itakuwa huru na inayojitegemea.

Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria imetoa taarifa ikisema ina wasiwasi na shaka kuhusu uhuru wa tume hiyo na inasisitiza kwamba, hadi sasa serikali ya Abuja haijaomba radhi rasmi wala kuchunguza mauaji ya halaiki yaliyofanywa na jeshi la nchi hiyo dhidi ya mamia ya Waislamu katika mji wa Zaria mwaka 2015. 

Jeshi la Nigeria limeaua mamia ya Waislamu Zaria, 2015

Wakati huo huo shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limetoa wito wa kupewa kinga watu watakaotoa ushahdi katika tume hiyo na kuhakikisha wahanga wa ukikwaji wa haki za binadamu wanatendewa haki na uadilifu.   

Tags