Muhammad Mursi ahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kushirikiana na Qatar
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i34455-muhammad_mursi_ahukumiwa_kifungo_cha_maisha_jela_kwa_kushirikiana_na_qatar
Mahakama moja nchini Misri imemuhukumu rais wa zamani wa Misri, Muhammad Mursi kifungo cha maisha jela.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 16, 2017 23:40 UTC
  • Muhammad Mursi ahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kushirikiana na Qatar

Mahakama moja nchini Misri imemuhukumu rais wa zamani wa Misri, Muhammad Mursi kifungo cha maisha jela.

Jumamosi ya jana mahakama hiyo ya Misri ilimuhukumu rais huyo aliyeuzuliwa madarakani na jeshi la nchi hiyo kifungo cha maisha kwa tuhuma ya kuifanyia ujasusi serikali ya Qatar na kusisitiza kuwa, hukumu hiyo ni ya mwisho isiyopasa kukatiwa tena rufaa. Kwa mujibu wa sheria za Misri, kifungo cha maisha ni cha miaka 25.

Mahkama ya nchini Misri

Kadhalika mahakama ya nchi hiyo imetoa hukumu ya adhabu ya kifo kwa viongozi watatu wa harakati ya Ikhwanul Muslimin iliyopigwa marufuku ndani ya taifa hilo la kaskazini mwa Afrika kwa tuhuma za kufanya ujasusi na kuwasilisha ripoti za siri kwa jeshi la Qatar. Baada ya Muhammad Mursi, kuondolewa madarakani mwaka 2013 kupitia mapinduzi ya kijeshi, shughuli za kundi la Ikhwanul Muslimin zilipigwa marufuku nchini humo huku viongozi wake wengi na wanachama wa kundi hilo wakitiwa jela na kuhukumiwa vifungo mbalimbali.