Waasi wadhibiti mji Bacaraga nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i34835-waasi_wadhibiti_mji_bacaraga_nchini_jamhuri_ya_afrika_ya_kati
Kundi la waasi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati limedhibiti mji wa Bacaraga, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 25, 2017 11:10 UTC
  • Waasi wadhibiti mji Bacaraga nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kundi la waasi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati limedhibiti mji wa Bacaraga, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Habari kutoka nchini humo zinaarifu kwamba, kundi la waasi la 'Kurejea kwenye Maridhiabo ya Kitaifa na Marekebisho' kwa kushirikiana na kundi la 'Harakati ya Kitaifa CAR' lilivamia mji huo kuanzia Jumamosi iliyopita na kuudhibiti kikamilifu. Kwa mujibu wa duru za kieneo, waasi hao wametwaa kwa nguvu magari ya taaisis za kibinaadamu na kuyatumia kuendeshea opresheni zao ndani ya mji wa Bacaraga. Kufuatia hali hiyo wakazi wa mji huo wamelazimika kuyahama makazi yao.

Jamhuri ya Afrika ya Kati

Hadi sasa serikali ya Bangui bado haijatoa radiamali yoyote kuhusiana na tukio hilo. Mapigano kati ya makundi ya wabeba silaha hasimu yameongezeka katika miezi ya hivi karibuni na kuwawafanya maelfu ya watu kuwa wakimbizi. Machafuko na vitendo vya ukatili nchini CAR vinajiri katika hali ambayo hadi sasa kuna askari elfu 10 wa Umoja wa Mataifa ndani ya taifa hilo la katikati mwa Afrika.