Ugonjwa wa tauni wauwa watu 124 Madagascar; miji mikubwa yatajwa kuathirika zaidi
Ugonjwa wa tauni nchini Madagascar umeuwa watu 24 tangu mwezi Agosti mwaka huu, katika mripuko unaoonekana kuiathiri zaidi miji miwili mikubwa ya kisiwa hicho kinachopatikana katika Bahari ya Hindi. Hayo yameelezwa leo na maafisa husika wa Madagascar.
Ugonjwa wa tauni umekuwa ikiikumba Madagascar mara kwa mara, hata hivyo mlipuko wa ugonjwa huo uliosababisha kushukiwa kuambukizwa watu 1,192 tangu mwezi Agosti mwaka huu ni wenye kutishia hofu mahususi kwa sababu ulianza mapema kabla ya wakati wa kawaida na umeathiri maeneo ya mijini kuliko ya vijijini.
Aidha imeelezwa kuwa, theluthi mbili za watu walioambukizwa ugonjwa huo wamepatwa na tauni ya pneumonia ambao inatajwa kuwa hatari sana. Ofisi ya Taifa ya kukabiliana na Majanga ya Madagascar imeeleza katika taarifa yake kuwa, idadi hiyo ya wagonjwa 1192 waliotajwa kuugua ugonjwa wa tauni inayoambatana na pneumonia ni mara tatu zaidi ikilinganishwa na wastani jumla wa watu wanaoambukizwa ugonjwa huo kila mwaka nchini humo.
Ripoti iliyotolewa wiki iliyopita Shirika la Afya Duniani (WHO) imeeleza kuwa watu 94 wameaga dunia kwa maradhi hayo huko Madagascar. Mji mkuu wa Madagascar, Antananarivo na ule wa Toamasina miji miwili mikubwa nchini humo ndiyo imeathirika zaidi na ugonjwa tauni huku asilimia 55 ya kesi zikisajiliwa katika miji hiyo. Wafanyakazi wa afya 54 wamekumbwa na ugonjwa huo hadi sasa.