Polisi nchini Tunisia waandamana, wataka kulindwa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i36155-polisi_nchini_tunisia_waandamana_wataka_kulindwa
Maafisa wa polisi nchini Tunisia wamefanya maandamano wakitaka kupitishwe rasimu ya muswada wa kuwalinda.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Nov 04, 2017 07:53 UTC
  • Polisi nchini Tunisia waandamana, wataka kulindwa

Maafisa wa polisi nchini Tunisia wamefanya maandamano wakitaka kupitishwe rasimu ya muswada wa kuwalinda.

Waandamanaji hao sambamba na kutoa nara huku wakiwa wameshikilia mabango, wametaka kufanyiwa marekebisho sheria ambayo inayaweka maisha ya polisi hatarini. Kadhalika maafisa hao wa polisi wamesisitizia umuhimu wa kuendelezwa mapambano dhidi ya ugaidi nchini. Maandamano hayo yamefanyika baada ya kuuawa polisi mmoja kwa kuchomwa kisu na gaidi mmoja hivi karibuni.

Bunge la Tunisia

Alkhamisi iliyopita afisa mmoja wa polisi alishambuliwa na gaidi karibu na jengo la bunge mjini Tunis, mji mkuu wa Tunisia na kupoteza maisha kutokana na majeraha makali aliyoyapata. Rasimu ya muswada wa sheria ya kuwalinda polisi, askari, maafisa usalama na maafisa wa forodha inatajwa kuwa njia inayoweza kudhamini usalama wa maafisa hao kutokana na hatari ya mashambulizi. Hata hivyo mashirika binafsi nchini Tunisia yanaitaja rasimu hiyo kuwa tishio kwa uhuru wa kujieleza na kuwasilisha maoni, hivyo yanapinga kupitishwa kwake.