Uzayuni wa kimataifa ndio uliofanya shambulizi la kigaidi Sinai Misri
Mchambuzi mkuu wa gazeti kubwa zaidi binafsi la nchini Misri amesema kuwa, Uzayuni wa kimataifa ndio uliohusika katika mauaji ya umati yaliyofanyika Ijumaa iliyopita katika msikiti mmoja mkubwa kwenye Rasi ya Sinai, kaskazini mwa Misri.
Abdul Nassir Salama, mchambuzi mwandamizi wa nchini Misri amesema katika mahojiano aliyofanyiwa na gazeti la al Masiratul Yaum la nchi hiyo kwamba utawala wa Kizayuni wa Israel unafanya njama za kila namna za kuwaondoa wakazi wa eneo la Sinai kama sehemu ya njama zake za kuliteka na kulikalia tena kwa mabavu eneo hilo la Misri.
Ameongeza kuwa, mauaji ya umati yaliyofanyika katika msikiti wa al Raudha yamepangwa na utawala wa Kizayuni wa Israel na hili ndilo suala la kutiliwa mkazo sana na kuamshwa watu kuhusu ukweli huo.
Mchambuzi huyo mkubwa wa masuala ya kisiasa nchini Misri amesisitiza kuwa, machafuko ya nchini Misri yanachochewa na utawala wa Kizayuni na yamepelekea kupungua uungaji mkono kwa Wapalestina suala ambalo ndilo lengo kuu la utawala ghasibu wa Israel.
Abdul Nassir Salama pia amesema, wachambuzi na wanafikra wengine wa Misri wanapaswa kulaumiwa kutokana na kukaa kimya na kutoilaani Israel kwa vitendo vyake viovu.
Ni vyema tukakumbusha hapa kwamba Waislamu 305 waliuawa kwa umati na makumi ya wengine kujeruhiwa baada ya magaidi kuwavamia Waislamu hao waliokuwa wanasali Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa al Rawdha kwenye mji wa al Arish, makao makuu ya mkoa wa Sinai Kasizini huko Misri.