Mar 21, 2018 07:43 UTC
  • Watu kadhaa wauawa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wameripoti kuwa watu wawili wameuawa na wawili wengine kujeruhiwa katika mapigano yaliyotokea baina ya watu wenye silaha kusini mwa nchi hiyo.

Kikosi cha Minusca kimetangaza kuwa, wanachama wawili wa kundi linalojiita Umoja kwa Ajili ya Jamhuri ya Afrika ya Kati wameuawa katika mapigano kati ya kundi hilo na wanamgambo wa Anti Balaka katika eneo la Alindao. 

Minusca imeongeza kuwa, wanajeshi wawili wa kikosi hicho mmoja raia wa Burundi na mwingine kutoka Gabon pia wamejeruhiwa katika ufuatuaji risasi uliojiri baina ya makundi hayo ya wanamgambo wenye silaha.

Jamhuri ya Afrika ya Kati imegubikwa na machafuko ya ndani yaliyoanza mwaka 2013 baada ya kuanza uasi wa kundi la wapiganaji wa Seleka uliochochewa na uingiliaji kijeshi wa Ufaransa na kisha kundi hilo limuondoa madarakani Rais wa wakati huo Francois Bozize. 

Waasi wa Seleka wa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati 

Makundi tofauti yanayobeba silaha katika mikoa mbalimbali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati yanapigana lengo likiwa ni kupora madini ya almasi, dhahabu na mifugo. 

Tags