Rais al-Bashir wa Sudan alifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i44464-rais_al_bashir_wa_sudan_alifanyia_mabadiliko_baraza_lake_la_mawaziri
Rais Omar Hassan al-Bashir amelifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri kufuatia mgogoro wa kiuchumi unaoikabili nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 14, 2018 03:12 UTC
  • Rais al-Bashir wa Sudan alifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri

Rais Omar Hassan al-Bashir amelifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri kufuatia mgogoro wa kiuchumi unaoikabili nchi hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Rais mjini Khartouum imesema kuwa, Rais al-Bashir amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri ambapo amewabadilisha mawaziri kumi na tatu na magavana kumi.

Hata hivyo taarifa hiyo imeeleza kuwa, maelezo zaidi kuhusiana na mabadiliko hayo ya baraza la mawaziri yatatolewa baadaye leo.

Itakumbukwa kubwa mwezi uliopita wa Aprili, Rais al-Bashir alimfuta kazi Ibrahim Ghandour aliyekuwa Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Sudan.

Maandamano ya kupinga serikali ya Rais al-Bashir baada ya maisha kuwa magumu

Aidha mwanzoni mwa mwezi huu, Rais Omar al Bashir wa Sudan aliagiza kuandaliwa upya muundo wa kitaasisi wa mabalozi wanaoiwakilisha nchi hiyo nje ya nchi na kufungwa balozi 13 za nchi hiyo kutokana na nchi hiyo kukabiliwa na mgogoro wa fedha.

Rais wa Sudan alichukua uamuzi huo ili kupunguza gharama za matumizi kwa kuzingatia hali ya kiuchumi na kuzidisha utendaji katika Wizara ya Mambo ya Nje.

Balozi 13 za uwakilishi wa kisiasa za Sudan nje ya nchi zitafungwa kwa mujibu wa agizo hilo la Rais Omar al Bashir; ambapo imeelezwa kuwa kutakuwepo na balozi mmoja tu katika jumla ya balozi saba huku balozi ndogo nne zikifungwa.

Gharama za maisha nchini Sudan ambazo zimepanda kwa asilimia 50 na kupelekea kuibukka mfumuko mkubwa wa bei za bidhaa zimezidisha malalamiko ya wananchi dhidi ya serikali.