May 16, 2018 13:40 UTC
  • UN yataka kuongezwa misaada ya kibinadamu nchini Sudan

Umoja wa Mataifa umeitaka jamii ya kimataifa kuongeza misaada ya kibinadamu kwa Sudan kutokana na hali ya kimaisha kuzidi kuwa mbaya nchini humo.

Mark Lukok, afisa wa masuala ya misaada ya kibinadamu na misaada ya dharura ya Umoja wa Mataifa amesema hayo baada ya kutembelea kambi moja ya wakimbizi katika eneo la Kordofan Kusini, kusini mwa Sudan na kusema kuwa watu zaidi ya milioni saba wanahitajia misaada ya dharura yenye thamani ya dola bilioni 104 huko Sudan.

Eneo la Kordofan Kusini

 

Mwezi Februari mwaka huu, Umoja wa Mataifa uliitisha kikao cha kujadili hali mbaya na mgogoro  mkubwa wa kiuchumi wa Sudan ambao unatishia kuzuka janga la kibinadamu nchini humo. Miongoni mwa sababu za hali hiyo mbaya na maisha ya wananchi wa Sudan ni kuadimika mafuta na kuongezeka bei za bidhaa za lazima.

Mapigano baina ya jeshi la Sudan na waasi katika maeneo mawili ya Kordofan na Blue Nile uko kusini mwa Sudan yalianza mwaka 2011 baada ya Sudan Kusini kutangaza kujitenga. Mapigano hayo yameshapelekea mamilioni ya watu kuwa wakimbizi hadi hivi sasa. 

Tags