Apr 06, 2016 02:54 UTC
  • Viongozi wa Wakristo Senegal watunukiwa zawadi ya Qur’ani Tukufu

Mwakilishi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa (SAW) nchini Senegal amekutana na viongozi wa Wakristo nchini humo na kuwakabidhi zawadi ya nakala ya Qur’ani iliyotarjumiwa kwa lugha ya Kifaransa.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Hujjjatul Islam wal Muslimin Abbas Muutaqidi, Mwakilishi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa (SAW) cha Iran akiwa ameandamana na Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini Senegal, hivi karibuni walifika katika Kanisa Kubwa (Cathedral) la mji mkuu wa nchi hiyo Dakar kwa ajili ya shughuli hiyo. Wakiwa hapo walimpa salamu za mwaka mpya wa Milladia Askofu Mkuu wa Dakar Benjamin Ndiaye na kumzawadia nakala ya Qur’ani Tukufu iliyotarjumiwa kwa Kifaransa.

Katika kikao hicho, Askofu Mkuu Ndiaye aliukaribisha kwa moyo mkunjufu ujumbe huo wa Iran na kubainisha furaha yake kuhusu mkutano huo.

Tags