Serikali ya Sudan yatakiwa kuondoa wanajeshi wake nchini Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i45714-serikali_ya_sudan_yatakiwa_kuondoa_wanajeshi_wake_nchini_yemen
Katibu Mkuu wa chama cha Kongresi ya Wananchi cha Sudan ameitaka serikali ya nchi hiyo kuwarejesha nyumbani wanajeshi wa Sudan wanaoshiriki katika mashambulizi ya kivamizi nchini Yemen.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 11, 2018 09:37 UTC
  • Serikali ya Sudan yatakiwa kuondoa wanajeshi wake nchini Yemen

Katibu Mkuu wa chama cha Kongresi ya Wananchi cha Sudan ameitaka serikali ya nchi hiyo kuwarejesha nyumbani wanajeshi wa Sudan wanaoshiriki katika mashambulizi ya kivamizi nchini Yemen.

Televisheni ya al Jazeera imemnukuu Ali al Haj akisema hayo mbele ya waandishi wa habari mjini Khartoum na kusisitiza kuwa, wananchi walio wengi wa Sudan wanataka wanajeshi wa nchi yao warejee nyumbani mara moja na wasiendelee na mashambulizi ya kivamizi huko Yemen.

Vile vile ameelezea wasiwasi wake kuhusiana na matukio ya kijeshi katika baadhi ya nchi za Kiarabu kama vile Syria, Iraq na Yemen na kutahadharisha kuwa, kitendo cha baadhi ya nchi za Kiarabu cha kuingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine hakina mwisho mwema.

Al-Tayyib Mustafa, mkuu wa chama cha Justice and Peace Platform cha nchini Sudan

 

Naye Al-Tayyib Mustafa, mkuu wa chama cha Justice and Peace Platform cha nchini Sudan ameitaka serikali ya nchi hiyo kuchukua maamuzi mazuri katika sera zake za nje hasa kuhusu nchi za pambizoni mwa Ghuba ya Uajemi.

Amesema, serikali ya Sudan inapaswa kuiunga mkono Qatar ambayo iliisaidia katika mgogoro wake wa Darfur.

Mwaka 2015 Sudan ilituma wanajeshi wake nchini Yemen kwa tamaa ya misaada ya kifedha ya Saudi Arabia.

Wananchi na viongozi mbalimbali wa nchi hiyo wamekuwa muda wote wakiilaumu serikali ya Rais Omar al Bashir na kuitaka iwarejeshe nyumbani wanajeshi wa Sudan wanaouawa ovyo nchini Yemen.