Tahadhari kuhusu harakati za Israel huko Darfur
Harakati ya Kongresi ya Taifa Ya Sudan imetahadharidha kuhusu uingiliaji wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika kuzusha machafuko na ghasia kwenye eneo la Darfur.
Katibu Mkuu wa Kongresi ya Taifa ya Sudan, Ali al Haj ametahadharisha kuhusu harakati za utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo la Jabar Murrah huko Darfur na kusema: Uingiliaji wa utawala huo na baadhi ya pande za kimataifa utazusha tena moto wa vita na mapigano katika eneo la Darfur. Amesema harakati hizo zinafanyika kwa shabaha ya kudhamini malengo ya Israel katika eneo hilo.
Ali al Haj ameitaka serikali ya Sudan kuchukua hatua za haraka za kuimarisha amani na kuzuia machafuko zaidi katika eneo la Darfur.
Eneo hilo limekuwa katika machafuko ya ndani kwa miaka kadhaa sasa na maelfu ya wakazi wake wamelazimika kuwa wakimbizi.
Wakazi wa Darfur wanaituhumu serikali kuu ya Sudan kuwa inawatenga na kuwabagua kiuuchumi na kisiasa na wamekuwa wakipigana na serikali ya Khartoum tangu mwaka 2003. Serikali ya Sudan ilisimamisha mapigano kwa upande mmoja katika eneo hilo tangu Juni mwaka 2016.