Watoto wa Nigeria wamuomboleza mtoto aliyeuawa shahidi katika shambulizi la Ahvaz
Kikundi kimoja cha watoto kimefanya matembezi ya amani katika mji mkuu wa Nigeria Abuja, kumkumbuka na kumuenzi mtoto wa miaka minne aliyeuawa shahidi katika shambulizi la kigadi la Ahvaz, kusini magharibi mwa Iran.
Habari zinasema kuwa, kikundi hicho cha watoto wa Nigeria kilifanya matembezi ya amani na kisha kukusanyika mjini Abuja jana Jumatatu, kwa ajili ya kumuomboleza mtoto huyo wa Kiirani aliyeua shahidi kwa jina Muhammad Twaha Aqdami aliyekuwa na umri wa miaka minne.
Watoto hao walikuwa wamebeba picha ya mtoto huyo aliyeuawa shahidi huku wengine wakiwa wamebeba mabango.
Baadhi ya mabango hayo yalikuwa na jumbe zinazosema: "Tunaomboleza na watu wa Ahvaz", na "Sisi sote ni Twaha".
Vyombo vya usalama nchini Iran vimesisitiza kuwa, taifa hili litatoa jibu kali kwa wahusika wa tukio chungu la Ahvaz kusini magharibi mwa Iran.