Wagombea watano kuchuana katika uchaguzi wa Rais wa Senegal
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i51680-wagombea_watano_kuchuana_katika_uchaguzi_wa_rais_wa_senegal
Senegal ambayo inatajwa kuwa nchi yenye demokrasia iliyoimarika zaidi magharibi mwa Afrika inajianda kwa ajili ya uchaguzi wa rais Jumapili ijayo huku rais wa sasa wa nchi hiyo Macky Sally akitazamia kuchuana kwenye kinyang'anyiro hicho na wagombea wengine wanne.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 20, 2019 10:48 UTC
  • Wagombea watano kuchuana katika uchaguzi wa Rais wa Senegal

Senegal ambayo inatajwa kuwa nchi yenye demokrasia iliyoimarika zaidi magharibi mwa Afrika inajianda kwa ajili ya uchaguzi wa rais Jumapili ijayo huku rais wa sasa wa nchi hiyo Macky Sally akitazamia kuchuana kwenye kinyang'anyiro hicho na wagombea wengine wanne.

Rais wa sasa wa Senegal anatazamiwa pakubwa kushinda muhula wa pili wa kiti cha urais katika uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Jumapili ijayo baada ya shakhsia wawili mashuhuri wa upinzani wa nchi hiyo kuzuiwa kushiriki kwenye uchaguzi huo kwa tuhuma za ubadhirifu. Hata hivyo wakosoaji wa serikali ya Senegal wameitaja hatua hiyo kuwa ni ukandamizaji wa kutisha dhidi ya wapinzani.  Rais Macky Sall wa Senegal kwa mara ya kwanza aliingia madarakani mwaka 2012 baada ya kumshinda katika duru ya pili ya uchaguzi rais wa kabla yake Abdoulaye Wade.   

Rais Macky Sall wa Senegal 

Sall mwenye umri wa miaka 57 alianza siasa akiwa mwanachama wa chama kilichokuwa kikiongozwa na Wade cha Senegalese Democratic Party (PDS) na kisha baina ya mwaka 2004 na 2007  akawa Waziri Mkuu wake. Hata hivyo mivutano ya ndani ilimfanya Sall ajitenge na Wade mwaka 2008 na akaamua kuunda chama chake kwa jina la Alliance for the Republic (APR).