Apr 17, 2016 04:25 UTC
  • Rais Mahama wa Ghana
    Rais Mahama wa Ghana

Rais John Dramani Mahama wa Ghana ameamuru kuchukuliwa hatua kali za kiusalama baada ya kuongezeka wimbi la mashambulizi ya kigaidi katika nchi za magharibi mwa Afrika.

John Dramani Mahama ameamuru kuchukuliwa hatua kali za kiusalama na dhidi ya ugaidi na amewataka wananchi wa Ghana kuwa tayari kwa ajili ya hatari ya aina yoyote ile.

Wito huo wa Rais wa Ghana umetolewa baada ya Baraza Kuu la Usalama wa Taifa kutahadharisha kwamba, ushahidi uliopo unaonesha kuwa, wanachama wa makundi ya kigaidi huko Ivory Coast wanapanga kufanya mashambulizi nchini humo. Nyaraka zilizopatikana zinaonesha kuwa magaidi wa al Qaida wanapanga kufanya mashambulizi katika nchi za Ghana na Togo.

Wiki kadhaa zilizopita magaidi waliokuwa wamefunika nyuso zao wa kundi la al Qaida walishambulia kwa risasi hoteli tatu nvhini Ivory Coast ikiwemo ile ya L’Etoile du Sud (Southern Star) katika ufukwe wa Grand Bassam mjini Abidjan na kuua watu 19.

Tags