Kundi la Haftar lapinga mazungumzo ya amani mpaka "liiteke" Tripoli
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i54107-kundi_la_haftar_lapinga_mazungumzo_ya_amani_mpaka_liiteke_tripoli
Aguila Saleh, Spika wa Bunge la Tobruk linalomuunga mkono Khalifa Haftar huko Libya amesema kuwa hawatoshiriki katika mazungumzo yoyote ya amani hadi pale watakaooipindua serikali ya Umoja wa Kitaifa na kuiteka Tripoli, mji mkuu wa Libya.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 13, 2019 22:03 UTC
  • Kundi la Haftar lapinga mazungumzo ya amani mpaka

Aguila Saleh, Spika wa Bunge la Tobruk linalomuunga mkono Khalifa Haftar huko Libya amesema kuwa hawatoshiriki katika mazungumzo yoyote ya amani hadi pale watakaooipindua serikali ya Umoja wa Kitaifa na kuiteka Tripoli, mji mkuu wa Libya.

Nchi ya Libya yenye utajiri mkubwa wa mafuta inaongozwa na serikali mbli hasimu, moja yenye bunge lake huko Tobruk na nyingine ya Tripoli inayotambuliwa na jamii ya kimtaifa ukiwemo Umoja wa Mataifa.

Bunge la Tobruk linamuunga mkono jenerali muasi Khalifa Haftar anayoongoza wanamgambo wanaojiita Jeshi la Taifa la Libya ambaye mapema mwezi Aprili mwaka huu alianzisha mashambulzi ya pande zote dhidi ya mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli, baada ya kutembelea Saudi Arabia na kufanya mazungumzo na viongozi wa nchi hiyo.

Mapigano nchini Libya hayana ishara ya kumalizika

 

Nchi nyingine zilizotangaza waziwazi kumuunga mkono Jenerali Haftar ni Umoja wa Falme za Kiarabu na Misri. Hata rais wa Marekani, Donald Trup alizungumza kwa simu na jenerali huyo muasi na kumwambia kuwa anaunga mkono juhudi zake za kupambana na "ugaidi" na kulinda "usalama" wa visima vya mafuta vya Libya.

Hata hivyo tofauti na matarajio ya Jenerali Haftar, kampeni yake ya kuuteka mji mkuu Tripoli inaonekana kukwama kutokana na muqawama mkubwa wa jeshi la Libya na waungaji mkono wa serikali ya umoja wa kitaifa ya nchi hiyo. Ijapokuwa Umoja wa Mataifa umepiga marufuku kupelekewa silaha makundi hasimu huko Libya, lakini mara kwa mara silaha na ndege za kivita za nchi za Kiarabu zinazomuunga mkono Jenerali Khalifa Haftar zimekuwa zikionekana kushiriki kwenye mashambulizi dhidi ya wakazi wa Tripoli.

Hii ni katika hali ambayo hivi karibuni, televisheni ya Rusia al Yaum ilimnukuu Farhan Haq, Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akisema kuwa, idadi ya watu waliokimbia makazi yao mjini Tripoli, Libya, kutokana na mapigano, imeongezeka na kupindukia 90 elfu na idadi hiyo inaongezeka siku baada ya siku.