Sudan yaomba msaada wa kimataifa kwa waathiriwa wa mafuriko
(last modified Tue, 08 Sep 2020 16:22:48 GMT )
Sep 08, 2020 16:22 UTC
  • Sudan yaomba msaada wa kimataifa kwa waathiriwa wa mafuriko

Waziri wa Afya wa Sudan ametahadharisha kuhusu uwezekano wa kujitokea maradhi ya kuambukiza katika siku kadhaa zijazo kutokana na maafa yaliyosababisha na mafuriko makubwa yanayoendelea nchini humo.

Waziri wa Afya wa Sudan amesema hayo baada ya mwakilishi wa nchi hiyo katika ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva kuziomba jumuiya za kimataifa kuchukua hatua za haraka za kuwasaidia watu waliokumbwa na mafuriko nchini Sudan.

Jumamosi iliyopita serikali ya Sudan ilitangaza hali ya hatari nchini humo kutokana na mafuriko makubwa ambayo yamua zaidi ya watu mia moja na kuharibu zaidi ya nyumba laki moja.

Wakati huo huo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hilali nyekundu la Sudan, Ahmad Zakaria amesema kuwa athari za mafuriko yaliyoikumba nchi hiyo zinaendelea kuongezeka siku baada ya nyingine na kwamba operesheni ya uokoaji na tathmini ya hasara za mafuriko hayo bado inaendelea.

Mafuriko ya Sudan

Mvua kali zinazoendelea kunyesha kusini na mashariki mwa mji mkuu wa Sudan, Khartoum zimesababisha mafuriko makubwa na hasara na mali na nafsi.

Mji wa Khartoum pia unaendelea kusumbuliwa na mafuriko kwa wiki ya pili sasa kutokana na kujaa mali ya Mto Nile. Mafuriko hayo yametajwa kuwa hayajawahi kushuhudiwa nchini Sudan kwa kipindi cha karne nzima iliyopita.

Tags