Makabiliano ya waandamanaji Waafrika wenyeji na Wazungu Afrika Kusini
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i64052-makabiliano_ya_waandamanaji_waafrika_wenyeji_na_wazungu_afrika_kusini
Wakulima wazingu na waandamanaji Waafrika wenyeji wamerushiana matusi katika maandamano siku ya Ijumaa nje ya mahakama wakati wa kusikilizwa kesi ya mauaji.
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
Oct 16, 2020 10:12 UTC
  • Maafisa wa polisi Afrika Kusini wakiwazuia waandamanaji wazungu kukabiliana na Waafrika
    Maafisa wa polisi Afrika Kusini wakiwazuia waandamanaji wazungu kukabiliana na Waafrika

Wakulima wazingu na waandamanaji Waafrika wenyeji wamerushiana matusi katika maandamano siku ya Ijumaa nje ya mahakama wakati wa kusikilizwa kesi ya mauaji.

Chuki za kibaguzi zimeibuka tena Afrika Kusini baada ya mzungu kupatikana ameuawa katika jimbo la Free State na kuibua maandamano na ghasia. Rais Cyril Ramaphosa alitoa taarifa na kuwataka watu wa Afrika Kusini kutokubali uchochezi kwa msingi wa ubaguzi wa rangi.

Wakulima wazungu, ambao wanadai serikali imeshindwa kuwalinda , waliwasili mahakamani katika mji wa Senekal wakiwa wamevalia sare za kijeshi kusikiliza kesi ya washukiwa wawili wa mauaji hayo.

Rais Cyril Ramaphosa

Wafuasi wa chama cha EFF, ambacho kinaungwa mkono na Waafrika Kusini wenyeji, ambao wanahisi hawajapata chochote hata baada ya kuangushwa mfumo wa ubaguzi wa rangi, wamejitokeza kwa maelfu wakati wa kusikilizwa kesi hiyo. Polisi wamelazimika kutenganisha makundi hayo mawili hasimu ili kuzuia ghasia na maafa. Chama cha EFF kinasema matatizo ya Afrika Kusini yanatokana na uchumi wa nchi hiyo kuendelea kushikiliwa na wazungu waliowachache. Karibu asilimia 70 ya ardhi binafsi za kilimo Afrika Kusini zinamilikiwa na wazungu ambao ni chini ya asilimi 9 ya watu wote milioni 58 nchini humo.