Haftar aamua kuvunja makundi ya wanamgambo mkoani Benghazi
Kundi linalojiiita jeshi la kitaifa la Libya linaloongozwa na Khalifa Haftar limetangaza kuwa limeandaa mpango wa kuyavunja makundi yenye silaha na kuondoka katika makazi yake katika mkoa wai Benghazi nchini humo.
Kundi hilo la wanamgambo wanaoongozwa na jenerali muasi Khalifa Haftar limetangaza kuwa makundi ya wanamgambo waliopo katika mkoa wa Benghazi yanavunjwa kwa amri ya Khalifa Haftar. Kikao kilichofanyika juzi Jumamosi cha Chumba cha Usalama wa Benghazi chini ya uongozi wa Abdulrazaq Mkuu wa jeshi la kitaifa la Libya kimefikia mapatano ya kuanzisha fremu ya utendaji kazi itakayosimamia uvunjwaji wa makundi hayo ya wanamgambo na kuwaondoa katika makazi yaliyokuwa chini yao.
Mikoa kadhaa ya Libya ukiwemo wa Benghazi bado inadhibitiwa na wanamgambo wa Khalifa Haftar.
Pande zinazozozana Libya yaani Serikali ya Wokovu wa Kitaifa yenye makao yake Tripoli na kundi kwa jina la jeshi la kitaifa la Libya chini ya uongozi wa Jenerali Khalifa Haftar tarehe 23 mwezi Oktoba mwaka huu zilisaini huko Geneva Uswisi mapatano ya kusimamisha vita yaliyosimamiwa na Umoja wa Mataifa.
Kwa msingi huo, mazungumzo ya kisiasa ya Walibya yatafanyika leo Jumatatu katika mji mkuu wa Tunisia. Katika mazungumzo hayo, pande hizo zitajadili na kubadilishana mawazo kuhusu namna ya kuendesha chaguzi za bunge na rais na kuunda serikali ya umoja wa kitaifa huko Libya.