Wagombea wa Baraza la Urais la Libya watangazwa
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Libya ametangaza orodha ya wagombea wa Baraza la Urais na kiti cha Waziri Mkuu nchini humo.
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Libya ametangaza orodha ya wagombea wa baraza la kiti cha urais ambayo ndani yake kunaonekana baadhi ya majina kama ya Khaled Ammar Al-Misri, Agila Saleh Qwaider na Salahuddin Al-Namroush; huku Ahmed Omar Ahmed Meitig, Osama Al-Sayd na Fathi Ali Abdul Salam Bashagha wakiarifishwa pia miongoni mwa wagombea wa nafasi ya Waziri Mkuu huko Libya.
Libya imekuwa ikikabiliwa na machafuko na ukosefu wa amani tangu kupinduliwa madarakani utawala wa kidikta wa Kanali Muammar Gaddafi mwaka 2011.
Weledi wa mambo wanaamini kuwa njia pekee ya kuhitimisha mgogoro wa Libya ni kufanyika uchaguzi na kuundwa serikali na jeshi lenye nguvu nchini humo.
Kwa kuzingatia hali ya mambo ilivyo huko Libya takwa kuu la wananchi pia ni kufanyika uchaguzi ambao utapelekea kuingia madarakani serikali yenye nguvu ili kuhitimisha hali mbaya ya sasa nchini humo.