Wanamgambo wa Haftar wapigana wao kwa wao katika mji wa Sirte, Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i66384-wanamgambo_wa_haftar_wapigana_wao_kwa_wao_katika_mji_wa_sirte_libya
Duru za habari zimearifu kuwa, wanamgambo wanaoongozwa na Jenerali muasi Khalifa Haftar kamanda wa vikosi kwa jina la jeshi la kitaifa la Libya wamepigana wao kwa wao katika mji wa Sirte huko Libya.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Feb 02, 2021 11:16 UTC
  • Wanamgambo wa Haftar wapigana wao kwa wao katika mji wa Sirte, Libya

Duru za habari zimearifu kuwa, wanamgambo wanaoongozwa na Jenerali muasi Khalifa Haftar kamanda wa vikosi kwa jina la jeshi la kitaifa la Libya wamepigana wao kwa wao katika mji wa Sirte huko Libya.

Duru za habari zimearifu kuwa, wanamgambo wa gadi  ya Tariq bin Ziyad huko mashariki mwa Libya leo Jumanne wamevamia makao ya wanamgambo wa kikosi cha tisa katika mji wa Sirte maarufu kwa jina la kikosi cha al Kaniyat. Duru hizo tajwa bila ya kutoa maelezo zaidi zimeeleza kuwa, silaha nyingin zimepelekwa katika eneo hilo kunakojiri mapigano.  

Libya imekumbwa na mgogoro wa kisiasa, ukosefu wa amani na hitilafu za ndani tangu kupinduliwa madarakani utawala wa dikteta Kanali Muammar Gaddafi. 

 Libya sasa ina serikali mbili. Moja ikiwa ni ile yenye makao yake huko Tripoli mji mkuu wa nchi hiyo chini ya uongozi wa Waziri Mkuu Fayez al Sarraj. Serikali hiyo inatambuliwa rasmi na kuungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

Fayez al Sarraj, Waziri Mkuu wa Serikali ya Libya inayotambuliwa rasmi na UN  

Na serikali ya pili ina makao yake katika mji wa Tobruk mashariki mwa nchi ikiungwa mkono na Imarati, Misri, Saudi Arabia na nchi kadhaa za Ulaya.