Waziri Mkuu mpya wa Libya apewa siku 21 kuunda serikali
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i66542-waziri_mkuu_mpya_wa_libya_apewa_siku_21_kuunda_serikali
Waziri Mkuu mpya wa Libya amepewa siku 21 kuwa ametangaza serikali mpya baada ya kupasishwa kwa wingi wa kura za baraza la mazungumzo ya amani ya Libya.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Feb 06, 2021 13:52 UTC
  • Waziri Mkuu mpya wa Libya apewa siku 21 kuunda serikali

Waziri Mkuu mpya wa Libya amepewa siku 21 kuwa ametangaza serikali mpya baada ya kupasishwa kwa wingi wa kura za baraza la mazungumzo ya amani ya Libya.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Libya Stephanie Williams amesema baada ya kuchaguliwa waziri mkuu na rais wa baraza la urais kuwa, hadi sasa bado kuna changamoto  nyingi na kwamba waziri mkuu wa muda wa Libya anapaswa kuunda serikali mpya katika kipindi cha siku 21 na kutangaza majina ya mawaziri wa serikali ili wapasishwa na bunge. 

Stephanie Williams ameongeza kuwa, iwapo waziri mkuu atashindwa kuarifisha mawaziri wa serikali katika kipindi kilichoainishwa, suala hilo litapelekwa katika baraza la mazungumzo ya amani ya Libya.

Mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa nchini Libya amesema kuwa baraza jipya la mawazi la Libya linapaswa kuwa na wawakilishi wa makundi yote wakiwemo vijana na wanawake. 

Katika hotuba yake ya kwanza baada ya kuchaguliwa, Waziri Mkuu wa Libya Abdulhamid al-Dabaiba alisema kuwa, baraza lake la mawaziri litaheshimu uwazi na uwajibikaji na litafanya juhudi kubwa za kutatua mtatizo ya nchi ikiwa ni pamoja na tatizo la umeme na kutayarisha chanjo ya corona.

Mohammed al-Menfi amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Baraza la Urais la Libya huku Abdulhamid al-Dabaiba akichaguliwa kuwa waziri mkuu katika zoezi ambalo lilisimamiwa na Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa ya jana. 

Uongozi huo mpya wa Libya utaitayarisha nchi hiyo kwa ajili ya uchaguzi wa bunge utakaofanyika Disemba 24.