Waziri Mkuu wa Libya atakiwa kuunda haraka serikali ya mpito
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i67234-waziri_mkuu_wa_libya_atakiwa_kuunda_haraka_serikali_ya_mpito
Baraza Kuu la Serikali ya Libya limemtaka Abdulhamid al-Dabaiba Waziri Mkuu wa nchi hiyo kuunda serikali yake haraka iwezekanavyo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Feb 25, 2021 03:51 UTC
  • Waziri Mkuu wa Libya atakiwa kuunda haraka serikali ya mpito

Baraza Kuu la Serikali ya Libya limemtaka Abdulhamid al-Dabaiba Waziri Mkuu wa nchi hiyo kuunda serikali yake haraka iwezekanavyo.

Baraza Kuu la Serikali ya Libya limetoa taarifa na kueleza kuwa, haliingilii kivyovyote katika uchaguzi wa wajumbe wa serikali ya umoja wa kitaifa na kwamba linataraji kuwa wajumbe wa serikali hiyo hatimaye watachaguliwa kwa uwazi kwa mujibu wa uwezo walionao.  

Baraza la Mazungumzo ya Libya lililofanyika huko Geneva chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa lilimchagua Abdulhamid al-Dabaiba kuwa Waziri Mkuu wa serikali ya mpito ya nchi hiyo, Mohamed Yunus al-Menfi kuwa Mkuu wa Baraza la Urais, na Abdullah Hussein Al Lafi na Musa Al Koni walichaguliwa kama wajumbe wawili wa baraza hilo. 

Waziri Mkuu wa serikali ya mpito ya Libya, Abdulhamid al Dadaiba 

Al Dabaiba alishinda kwa kura 39 na kuwapiku wapinzani wake akiwemo Aguila Saleh. 

Shakhsia hao wa Libya walioibuka na ushindi wana jukumu la kusimamia masuala ya Libya kwa muda hadi kutakapoitishwa chaguzi za rais na bunge Disemba 24 mwaka huu.