Hamas yataka kuungwa mkono Muhammad al Qiq
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i766-hamas_yataka_kuungwa_mkono_muhammad_al_qiq
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imewatolea mwito wananchi wa Palestina kushiriki kwa wingi katika maandamano ya kumuunga mkono mwandishi habari wa Kipalestina aliyeko katika jela ya Israel huku akiwa amegoma kula.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 07, 2016 04:19 UTC
  • Hamas yataka kuungwa mkono Muhammad al Qiq

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imewatolea mwito wananchi wa Palestina kushiriki kwa wingi katika maandamano ya kumuunga mkono mwandishi habari wa Kipalestina aliyeko katika jela ya Israel huku akiwa amegoma kula.

Kufuatia kuwa mbaya hali ya kimwili ya Muhammad al Qiq mwandishi habari wa Kipalestina kutokana na kuendelea kwake kugoma kula chakula, harakati ya muqawama ya Hamas imewataka wananchi wa Palestina kushiriki katika maandamano ya leo ili kuonyesha kumuunga mkono al Qiq na pia kuonyesha mshikamano kwa wafungwa wengine wa Kipalestina walioko katika jela za utawala wa Kizayuni wa Israel.

Hamas imevitolea wito vyombo vyote vya habari vya Palestina kuonyesha mshikamano wao kwa Muhammad al Qiq.

Taarifa ya Hamas imeongeza kuwa kudhurika kwa aina yoyote ile Muhammad al Qiq kutapelekea kushtadi Intifadha ya Quds na kusisitiza kuwa adui Mzayuni atagharimika kutokana na miamala yake ya kidhulma dhidi ya wafungwa wa Kipalestina. Muhammad al Qiq amegoma kula chakula tangu Novemba 25 mwaka jana akilalamikia mateso na miamala mibovu anayofanyiwa na utawala wa Kizayuni wakati wa kusailiwa.