Kiongozi wa Ikhwanul Muslimin Misri ahukumiwa kifungo cha maisha jela
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i8131-kiongozi_wa_ikhwanul_muslimin_misri_ahukumiwa_kifungo_cha_maisha_jela
Mahakama ya Misri imemhukumu kifungo cha maisha jela kiongozi wa harakati ya Ikhwanul Muslimin ya nchini humo na kuwahukumu vifungo tofauti jela wanachama wengine wa harakati hiyo iliyopigwa marufuku baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika na maandamano yaliyofanywa baada ya kupinduliwa Rais halali wa nchi hiyo Mohamed Morsi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 30, 2016 11:12 UTC
  •  Kiongozi wa Ikhwanul Muslimin Misri ahukumiwa kifungo cha maisha jela

Mahakama ya Misri imemhukumu kifungo cha maisha jela kiongozi wa harakati ya Ikhwanul Muslimin ya nchini humo na kuwahukumu vifungo tofauti jela wanachama wengine wa harakati hiyo iliyopigwa marufuku baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika na maandamano yaliyofanywa baada ya kupinduliwa Rais halali wa nchi hiyo Mohamed Morsi.

Maafisa wa mahakama wa Misri leo wameeleza kuwa Mohamed Badie na wenzake 35 wamepatikana na hatia ya kushiriki katika ghasia katika mji wa Ismailiya katika mfereji wa Suez, ghasia zilizosababisha vifo vya watu watatu mwezi Julai mwaka 2013. Mahakama hiyo ya Misri imewapata na hatia na kuwahukumu wanachama wengine 48 wa Ikhwan vifungo vya jela kuanzia miaka mitatu hadi 15. Katika upande mwingine mahakama hiyo pia leo imewaachia huru watu wengine 20 ambao walikuwa washtakiwa kwenye kesi hiyo. Mahakama za kijeshi za Misri zimekuwa zikikosolewa kwa kutoa hukumu kali.