UN yabainisha wasiwasi wake kuhusu haki za binadamu huko Senegal
(last modified Wed, 14 Jun 2023 04:41:01 GMT )
Jun 14, 2023 04:41 UTC
  • UN yabainisha wasiwasi wake kuhusu haki za binadamu huko Senegal

Umoja wa Mataifa umeeleza wasiwasi wake mkubwa kuhusu hali ya haki za binadamu huko Senegal.

Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa imetoa taarifa ikieleza wasiwasi wa umoja huo kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Senegal na kutangaza kuwa hatua ya askari usalama wa Senegal ya kutumia silaha moto dhidi ya waandamanaji inaitia doa jeusi nchi hiyo. 

Polisi wa Senegal wakikabiliana na waandamanaji 

Tangazo lililotolewa na Ofisi ya Kamisha Mkuu wa Haki za Binadamu wa UN linaeleza kuwa, watu wasiopngua 16 waliuawa, 350 kujeruhiwa na zaidi ya 500 kutiwa mbaroni katika maandamano ya siku tatu yaliyofanyika huko Senegal kati ya tarehe Mosi hadi tatu mwezi huu wa Juni.  

Senegal ilikumbwa na machafuko makubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini humo katika miaka ya karibuni kuanzia  tarehe Mosi hadi tatu mwezi huu wa Juni baada ya Ousmane Sonko, mmoja wa viongozi watajika wa upinzani, kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela katika kesi ya kimaadili.  

Viongozi wa Senegal walitangaza kuwa watu 16 wameuawa katika ghasia hizo. hata hivyo Amnesty International ilikadiria kuwa idadi ya watu waliopoteza maisha katika ghasia hizo ni 23.