-
Mahakama yaagiza mwili wa Edgar Lungu kurejeshwa Zambia
Aug 08, 2025 23:00Mahakama ya Afrika Kusini imeamua kuwa, serikali ya Zambia inaweza kuurejesha nyumbani mwili wa rais wa zamani Edgar Lungu na kumfanyia mazishi ya kitaifa, licha ya upinzani wa familia yake.
-
Jamii ya Wangazija yapiganiwa itambuliwe rasmi nchini Kenya
Aug 08, 2025 08:09Seneta wa Kaunti ya Mombasa iliyoko eneo la pwani ya Kenya ametoa wito wa kutaka suala la jamii ya Wangazija kutatuliwa na kupewa haki kama watu wengine nchini humo.
-
Mabadiliko ya baraza la mawaziri DRC yawaingiza wapinzani serikalini
Aug 08, 2025 04:13Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amelifanyia mabadiliko baraza la mawaziri na kuwateua viongozi kadhaa wa upinzani, kwa mujibu wa amri zilizosomwa kwenye televisheni ya taifa.
-
Ajali ya ndege ya matibabu nchini Kenya yaua watu sita na kujeruhi wawili
Aug 07, 2025 23:56Ndege ya shirika la huduma ya ambulensi ya anga ilianguka katika eneo la makazi ya watu nje kidogo ya mji mkuu wa Kenya, Nairobi jana Alhamisi, na kuua watu wasiopungua sita.
-
Wahamiaji 7 wa Ethiopia wameaga dunia kwa njaa na kiu wakielekea Yemen
Aug 07, 2025 23:07Wahamiaji saba wa Ethiopia wameaga dunia kutokana na njaa na kiu baada ya boti waliyokuwa wakisafiri kuharibika njiani wakitoka Somalia kuelekea Yemen.
-
Wafuasi wa Rais wa Tunisia waandamana dhidi ya Muungano Mkuu wa Wafanyakazi (UGTT)
Aug 07, 2025 23:00Mamia ya wafuasi wa Rais Kais Saied wa Tunisia jana waliandamana nje ya makao makuu ya Muungano Mkuu wa Wafanyakazi wa Tunisia (UGTT) na kumtaka kiongozi huyo kusimamisha muungano huo kufuatia mgomo wa sekta ya usafirishaji wiki iliyopita ambao umeilemaza nchi.
-
Umoja wa Mataifa: Kundi la M23 liliua watu 319 DRC mwezi Julai
Aug 07, 2025 08:28Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, waasi wa M23 waliua watu zaidi ya 300 katika mwezi uliopita wa Julai katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
-
Jeshi la Sudan lawaua wapiganaji 40 mamluki wa Colombia
Aug 07, 2025 08:27Jeshi la anga la Sudan limetangaza kuwa, limeiharibu ndege ya Imarati iliyokuwa imewabeba wapiganaji mamluki wa Colombia wakati ilipokuwa ikitua katika uwanja wa ndege unaodhibitiwa na jeshi huko Darfur, na kuwaua watu wapatao 40.
-
Mgomo wa madaktari Kenya wakaribia, muungano wake watoa siku 14 kwa serikali
Aug 07, 2025 08:26Sekta ya huduma za afya nchini Kenya, kwa mara nyingine inakabiliwa na mzozo baada ya Muungano wa Madaktari, Wafamasia na Madaktari wa Meno (KMPDU) kutoa notisi ya siku 14 ya mgomo kutokana na kile inachosema kutotiliwa maanani kwa makubaliano waliyotiliana saini kati ya serikali ya kitaifa na zile za kaunti.
-
Je, Afrika Kusini inafanya nini kukabiliana na ushuru mpya wa kibiashara wa Marekani?
Aug 07, 2025 04:49Wizara ya Biashara ya Afrika Kusini imetangaza kuwa imechukua hatua kadaa mpya za kukabiliana na ushuru mpya wa kibiashara wa Marekani.