-
Waziri Mkuu wa Sudan: Mazungumzo ya ndani kwa ajili ya maridhiano kuanza hivi karibuni
Aug 17, 2026 09:55Waziri Mkuu wa Sudan, Kamil Idris ametangaza kuwa, mazungumzo ya ndani kati ya makundi mbalimbali ya Wasudan yataanza hivi karibuni, kwa lengo la kufikia maridhiano ya kina nchini humo na hatimaye kufanyika uchaguzi huru na wa haki.
-
Katiba DRC: Muungano wa upinzani wa C64 waanza tena mvutano na serikali
Aug 17, 2026 06:01Mvutano wa kisiasa umeibuka tena katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya muda wa mwisho uliotolewa na wapinzani kumalizika siku ya Jumamosi, Agosti 15.
-
Mali yataka Afrika ijitegemee katika teknolojia za usalama
Aug 17, 2026 05:56Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali, Abdoulaye Diop, ametoa wito kwa nchi za Afrika kujenga uwezo wa kujitegemea katika teknolojia za ulinzi na usalama, badala ya kutegemea vifaa na teknolojia kutoka mataifa ya kigeni.
-
Rais wa Afrika Kusini asema, mashambulizi dhidi ya raia wa kigeni yameiaibisha nchi yake
Aug 16, 2026 09:50Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema, nchi yake "ina wasiwasi na aibu kubwa" kwa jinsi vikundi vya wanamgambo walivyowatendea raia wa kigeni wakati wa maandamano ya hivi karibuni ya kupinga wahamiaji yaliyowalazimisha maelfu kukimbia nchi.
-
UN: Ebola inaua mtu mmoja kila baada ya nusu saa huko Congo DR
Aug 16, 2026 03:17Tom Fletcher, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Masuala ya Kibinadamu, ametangaza kwamba mlipuko wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo sasa unaua mtu mmoja kila baada ya nusu saa, akitoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua za haraka kupambana na mlipuko huo.
-
Mkuu wa Baraza la Uongozi Sudan: Jeshi liko tayari kwa amani; apinga kurejea madarakani RSF
Aug 16, 2026 03:12Mkuu wa Baraza la Uongozi la Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, amesema kuwa jeshi bado limedhamiria kuwashinda wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF)—kikosi cha kijeshi kisicho rasmi- na amesisitiza kuwa jeshi liko tayari kupokea kile alichokiita juhudi za "kweli" za amani.
-
UN: Kikomboleo cha dola milioni 50 kilichochea mashambulizi ya Al-Qaeda nchini Mali
Aug 16, 2026 03:07Umoja wa Mataifa umearifu kuwa fedha za kikomboleo takriban dola milioni 50, zilizolipwa mwishoni mwa mwaka 2025 ili kuwaachia huru mateka nchini Mali, zilisaidia kufadhili wanamgambo wenye uhusiano na mtandao wa kigaidi Al-Qaeda na hujuma zao katika eneo zima la magharibi mwa Afrika.
-
Umoja wa Mataifa: Wakimbizi 650,000 Sudan Kusini hatarini kukosa chakula
Aug 15, 2026 10:54Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuwa zaidi ya wakimbizi 650,000 Sudan Kusini wako hatarini kukosa chakula katka wiki chache zijazo.
-
Uturuki yaitaka Tunisia imuachie kiongozi wa chama cha Kiislamu cha Ennahda anayesota gerezani
Aug 15, 2026 03:51Spika wa Bunge la Uturuki, Numan Kurtulmus, ametoa wito wa kutaka kiongozi wa chama cha Kiislamu cha Ennahda na Spika wa zamani wa Bunge la Tunisia, Rached Ghannouchi, ambaye anaendelea kusota gerezani, apatiwe matibabu na kuachiwa kwa kuzingatiwa utu na ubinadamu.
-
Mlipuko wa Ebola Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wasambaa hadi mkoa wa sita
Aug 14, 2026 10:06Mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umeenea hadi mkoa wa sita, baada ya kifo kimoja kurekodiwa katika mkoa wa Bas-Uele, ambao hapo awali haukuwa umeathiriwa na mlipuko huo.