-
Kenya yasimama na Morocco mgogoro wa Sahara Magharibi
May 27, 2025 03:03Kenya imesema inaunga mkono mpango wa Morocco wa kulipa eneo linalozozaniwa la Sahara Magharibi uhuru wa kujitawala chini ya mamlaka ya utawala wa kifalme wa nchi hiyo ya Afrika Kaskazini, ikiungana na idadi inayoongezeka ya nchi za Kiafrika, Kiarabu na Magharibi ambazo zimeelekeza uungaji mkono wao kwa Rabat katika mzozo huo wa miongo mitano.
-
Rais wa zamani wa DRC Joseph Kabila awasili Goma
May 26, 2025 23:25Joseph Kabila Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amewasili katika mji wa Goma wa mashariki mwa nchi hiyo licha ya kutuhumiwa kushirikiana na makundi ya waasi.
-
Afrika Kusini yaadhimisha Siku ya Afrika kwa mwito wa umoja na ushirikiano
May 26, 2025 06:52Afrika Kusini jana Jumapili iliadhimisha Siku ya Afrika kwa mwito wa kusisitizia umoja na ushirikiano wa kikanda na mshikamano wa kiutamaduni kwenye bara zima.
-
Rais wa Zambia atoa wito wa mshikamano na amani Afrika
May 26, 2025 03:43Rais Hakainde Hichilema wa Zambia, siku ya Jumapili alitoa wito wa mshikamano wa Kiafrika na maendeleo jumuishi wakati bara la Afrika likiadhimisha miaka 62 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), ambao sasa ni Umoja wa Afrika (AU).
-
Uganda yasimamisha ushirikiano wa kijeshi na Ujerumani
May 26, 2025 02:46Jeshi la Ulinzi la Uganda (UPDF) limetangaza kusitisha kwa muda ushirikiano wa kijeshi na wa kiulinzi na Ujerumani, kutokana na mwenendo usioridhisha wa balozi wa Ujerumani nchini humo.
-
Ethiopia yathibitisha kesi za kwanza za Ugonjwa wa Mpox katika mji unaopakana na Kenya na Somaliaa
May 26, 2025 02:37Ethiopia imethibitisha kesi zake za kwanza za ugonjwa wa mpox, zikihusisha mtoto mchanga wa siku 21 na mama yake, katika mji wa Moyale ulioko mpakani kusini mwa nchi, kwa mujibu wa taarifa ya mamlaka za afya iliyotolewa Jumapili.
-
Kwa nini Trump anasema uongo kuhusu mauaji ya watu weupe nchini Afrika Kusini?
May 26, 2025 02:31Senzo Mchunu, Waziri wa Polisi wa Afrika Kusini amefichua uongo wa Rais Donald Trump wa Marekani kuhusu mauaji ya wakulima wa kizungu nchini Afrika Kusini, na kusema: "Katika robo ya kwanza ya mwaka huu, jumla ya mauaji sita yanayohusiana na ardhi yalitokea Afrika Kusini, ambapo watano kati yao walikuwa watu weusi."
-
Joseph Kabila kuitembelea Goma hivi karibuni
May 25, 2025 22:47Joseph Kabila Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amesema anapanga hivi karibuni kutembelea mji wa Goma unaodhibitiwa na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda.
-
Mkutano wa kuadhimisha Siku ya Afrika wafanyika Addis Ababa
May 25, 2025 07:48Mkutano wa kuadhimisha Siku ya Afrika ulifanyika katika makao makuu ya Umoja wa Afrika (AU) huko Addis Ababa, Ethiopia, siku ya Jumamosi.
-
Kesi 2,500 za kipindupindu zaripotiwa chini ya mwezi mmoja mjini Khartoum pekee
May 25, 2025 03:37Waziri wa Afya wa Sudan, Haitham Mohamed Ibrahim ametangaza kuwa, wimbi kubwa la kipindupindu limeukumba mji mkuu Khartoum kiasi kwamba takriban kesi 2,500 za ugonjwa huo zimeripotiwa katika kipindi cha chini ya mwezi mmoja yaani ndani ya mwezi huu wa Mei tena mjini Khartoum pekee.