-
Libya yafunga bomba la mafuta karibu na mji wa Zawiya
May 25, 2025 03:21Shirika la Taifa la Mafuta la Libya (NOC) linalomilikiwa na serikali ya Libya inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa limetangaza kuwa limelazimika kufunga bomba la mafuta baada ya kugundua kupasuka na kuvuja mafuta huko kusini mwa Zawiya, yapata kilomita 45 magharibi mwa mji mkuu Tripoli.
-
Ethiopia yawapiga chanjo ya surua zaidi ya watoto milioni 11
May 24, 2025 22:50Ethiopia imeshawapiga chanjo watoto zaidi ya milioni 11 kama sehemu ya kampeni ya taifa zima ya kudhibiti ugonjwa wa surua unaoendelea kulisumbua taifa hilo.
-
Mauritius: Kurejea kwetu visiwa vya Chagos kutoka kwa mkoloni Uingereza, ni ushindi mkubwa
May 24, 2025 08:42Waziri Mkuu wa Mauritius, Navin Ramgoolam amesema kuwa, kufanikiwa nchi hiyo kuvirejesha kwenye milki yake visiwa vya Chagos kutoka kwa mkoloni Uingereza, ni ushindi mkubwa na wa kihistoria kwa taifa la Mauritius.
-
Kabila: Mfumo wa sheria wa DRC unavunda
May 24, 2025 04:17Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila jana Ijumaa ameshutumu vikali mfumo wa sheria wa nchi hiyo ya Afrika ya Kati, akisema kuwa umeoza kutokana na uendeshaji mbaya.
-
Jeshi la Nigeria lashadidisha operesheni dhidi ya Boko Haram
May 24, 2025 03:32Jeshi la Nigeria limesema kuwa limewaangamiza wanachama 16 wa kundi la kigaidi la Boko Haram katika jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa nchi, huku operesheni dhidi ya magaidi hao zikichachamaa.
-
Sudan: Imarati ilipanga njama za kumuua Abdel Fattah al-Burhan
May 23, 2025 23:03Sudan imeutuhumu Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwa kujaribu kumuua mkuu wa Baraza la Mpito Abdel Fattah al-Burhan, huko Port Sudan.
-
Bunge la Seneti DRC lamuondolea Joseph Kabila kinga ya kutoshtakiwa
May 23, 2025 08:53Bunge la Seneti la katika Jamhuri ya Kidemokkrasia ya Congo limeondoa kinga ya kutoshtakiwa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Joseph Kabila, na kuufuungua njia ya kufunguliwa mashtaka dhidi yake.
-
Waafrika Kusini wamjia juu Trump kwa kuongopa kwenye kikao na Ramaphosa
May 23, 2025 08:25Wananchi wa Afrika Kusini wameeleza kughadhabishwa na madai ya uwongo yaliyobuliwa na Rais wa Marekani Donald Trump wakati wa mazungumzo yake na Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini katika Ikulu ya White House.
-
AU haiwezi kufurahishwa na njama za kuwapora Wapalestina na kuwapeleka barani Afrika
May 23, 2025 02:55Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola Tete Antonio amesema kuwa, Umoja wa Afrika (AU) hauwezi kuwa na furaha unapoona kuna njama za kuwapora Wapalestina ardhi zao na kuwapeleka barani Afrika.
-
Umoja wa Mataifa waonya kuhusu hali mbaya ya kibinadamu nchini Sudan
May 23, 2025 02:55Umoja wa Mataifa jana Alkhamisi ulionya kuhusu hali mbaya ya kibinadamu inayozidi kuwa kali katika nchi ya Sudan iliyoharibiwa vibaya na vita vya uchu wa madaraka baina ya majenerali wa kijeshi.