-
Watu wanne wafariki Rwanda na hekari 70 za mazao zaharibika kufuatia mvua kubwa
Apr 15, 2025 06:41Watu wanne wamepoteza maisha yao na angalau hekari 70 za mazao zimeharibika ati ya Aprili 10 na 13, kufuatia mvua kubwa zilizosababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi nchini Rwanda. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya Wizara ya Usimamizi wa Masuala ya Dharura.
-
UN: Mauaji ya mamia ya watu El-Fasher, Sudan yanatisha
Apr 15, 2025 04:29Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amelaani vikali mashambulizi mabaya ya hivi karibuni ya Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) huko eneo la Darfur Kaskazini nchini Sudan akisema kuwa, mashambulizi hayo yanaashiria kushindwa kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua za maana licha ya maonyo ya mara kwa mara.
-
A/Kusini: Russia ni mshirika wetu mkuu katika sekta ya anga za mbali
Apr 14, 2025 23:44Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Kitaifa la Anga za Mbali la Afrika Kusini (SANSA) amesema Russia ni mshirika mkuu wa Afrika Kusini katika kuendeleza mipango yake ya kitaifa ya anga za juu.
-
Mkuu wa Kamisheni ya AU atoa mwito wa kukomeshwa mapigano nchini Sudan
Apr 14, 2025 23:43Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC), Mahmoud Ali Youssouf ameelezea wasiwasi wake kuhusu kuongezeka ghasia nchini Sudan, hasa katika eneo la Darfur Kaskazini.
-
Mhadhiri Ghana: Kimya cha dunia kwa jinai za Israel Gaza kinaaibisha
Apr 14, 2025 09:59Mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Ghana,Mustapha Abdullah Kuyateh amelaani vikali hujuma za kikatili za Israel dhidi ya Gaza, akisisitiza kuwa huo ni mwendelezo wa mauaji ya kimbari na mauaji ya halaiki dhidi ya Wapalestina.
-
Algeria yawapa wanadiplomasia wa Ufaransa saa 48 waondoke nchini humo
Apr 14, 2025 09:39Mvutano wa kidiplomasia kati ya Algeria na Ufaransa umezidi kupamba moto huku serikali ya Algiers ikiwataka wanadiplomasia 12 wa mkoloni huyo wa zamani wa Ulaya kuondoka nchini humo ndani ya saa 48.
-
Makumi wauawa katika shambulio la wabeba silaha Nigeria
Apr 14, 2025 09:38Zaidi ya watu 40 wameuawa katika shambulio la usiku wa manane dhidi ya jamii ya Zike huko Bassa, Jimbo la Plateau, huku mashambulio makali ya makundi yenye silaha yakiendelea kuripotiwa katika eneo hilo la kaskazini ya kati mwa Nigeria.
-
Mashambulio ya siku tatu mtawalia ya RSF yaua watu 450 Darfur, magharibi mwa Sudan
Apr 14, 2025 02:41Harakati ya Jeshi la Ukombozi wa Sudan, inayoongozwa na Minni Arko Minnawi (SLA-Minnawi), gavana wa jimbo la Darfur magharibi mwa nchi hiyo, imetangaza kuwa watu 450 wameuawa kutokana na mashambulizi ya siku ya tatu mtawalia yaliyofanywa na wapiganaji wa Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF) katika mji wa El Fasher, makao makuu ya eneo hilo, na kwenye kambi za wakimbizi.
-
Oligui Nguema ashinda kwa kishindo uchaguzi wa rais wa Gabon kwa kupata 90.35% ya kura
Apr 14, 2025 02:40Brice Oligui Nguema, kiongozi wa serikali ya mpito ya Gabon na mwanajeshi aliyeongoza mapinduzi ya mwaka 2023, amepata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa rais wa nchi hiyo wa 90.35% ya kura. Hayo ni kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani jana Jumapili.
-
Uhusiano na mkoloni Ufaransa wazidi kuharibika, Algeria yamwita balozi
Apr 13, 2025 22:52Wizara ya Mambo ya Nje ya Algeria imemwita balozi wa Ufaransa mjini Algiers, Stephane Romatet ili kujieleza ikiwa ni kuonesha malalamikio makali ya Algiers kuhusu kuzuiliwa balozi mdogo wa Algeria nchini Ufaransa.