-
Umoja wa Afrika wamemteua Rais wa Togo kupatanisha mgogoro wa DRC
Apr 06, 2025 09:38Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Joao Lourenco, amemteua Rais wa Togo, Faure Gnassingbe, kuwa mpatanishi kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Rwanda, na waasi wa M23.
-
Jeshi la Somalia laua magaidi 80 wa Al Shabab
Apr 06, 2025 09:19Vikosi vya usalama vya Somalia vimewaua zaidi ya magaidi 80 wa al-Shabaab, wakiwemo vinara waandamizi wa kundi hilo, katika operesheni za wiki nzima dhidi ya kundi hilo lenye mafungamano na mtandao wa kigaidi al-Qaeda.
-
Sakata la uuzaji wa Msikiti mkongwe zaidi Kenya
Apr 05, 2025 22:59Msikiti wa kihistoria wa Kongo, ulioko Diani, Kaunti ya Kwale, umekuwa katika mzozo baada ya mwekezaji binafsi kudai umiliki wa ardhi hiyo na kupewa hatimiliki mnamo Februari 17, 2025.
-
Kenya: Suluhisho la kudumu kwa mzozo wa DRC linapaswa kuwa la ndani
Apr 05, 2025 22:57Spika wa Bunge la Kitaifa la Kenya, Moses Wetang'ula, amesema kwamba suluhisho la kudumu kwa mzozo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) linapaswa kuwa la ndani, likizingatia mapendekezo kutoka kwa nchi za eneo.
-
Umoja wa Afrika wapigia debe Akili Mnemba kuleta mabadiliko
Apr 05, 2025 22:56Katika Mkutano wa Kimataifa kuhusu Akili Mnemba (Artificial Intelligence-AI-)barani Afrika, Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Mahmoud Ali Youssouf, ametangaza dhamira ya AU kuiweka Afrika kama kinara katika mapinduzi ya kimataifa ya akili mnemba.
-
Yamkini Facebook ikatozwa faini ya dola bilioni 2 ikipatikana na hatia ya kuchochea vita
Apr 05, 2025 22:51Mahakama Kuu ya Kenya imetoa uamuzi kwamba kampuni ya Marekani ya Meta, inayomiliki Facebook, inaweza kushtakiwa nchini humo kwa tuhuma za kuchochea chuki iliyopelekea vita vya kikabila nchini Ethiopia. Kesi hiyo, inayodai fidia ya dola bilioni 2.4, (takriban shilingi trilioni 3 za Kenya kwa makadirio ya sasa) imewasilishwa na watafiti wa Ethiopia na wanaharakati wa haki za binadamu wa Kenya.
-
Senegal yaadhimisha siku ya uhuru kwa mara ya kwanza bila ya uwepo mkubwa wa Ufaransa
Apr 05, 2025 07:20Senegal iliadhimisha miaka 65 ya uhuru jana Ijumaa ikiwa ni mara ya kwanza kwa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika kuadhimisha siku hiyo bila ya uwepo mkubwa wa wakoloni wa Ulaya yaani Ufaransa.
-
Watu wanaoshukiwa kuwa na silaha wameua watu 52 nchini Nigeria
Apr 05, 2025 07:19Takriban watu 52 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya magenge yenye silaha kufanya mashambulizi katikati mwa Nigeria.
-
Shirika la Msalaba Mwekundu lakanusha kuhusika na ndege iliyoshambuliwa DRC
Apr 05, 2025 05:33Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) imekanusha kuhusika kivyovyote vile na ndege ya misaada ya kibinadamu iliyoshambuliwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kusababisha kifo cha mtu mmoja.
-
Wapinzani CAR waandamana kupinga muhula wa tatu wa Rais Touadéra
Apr 05, 2025 03:40Maelfu ya waandamanaji wamemiminika katika mitaa ya Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wakiandamana bega kwa bega na wabunge wa upinzani kupinga vikali taarifa kwamba Rais Faustin-Archange Touadéra wa nchi hiyo anafanya juhudi za kuwania kiti cha urais kwa muhula wa tatu.