-
Iran: Yaishitaki Marekani kwa hatua yake ya kuiwekea vikwazo vipya Tehran
Aug 01, 2017 09:44Spika wa Majilisi ya Ushauri ya Kiislamu yaani Bunge la Iran sambamba na kubainisha kwamba, ukiukaji wa makubaliano ya nyuklia yanayojulikana kwa kifupi kama JCPOA uliofanywa na Marekani uko wazi, amesema kuwa Jamhuri ya Kiislam ya Iran imewasilisha mashitaka kwenda kwa baraza na kamisheni inayosimamia makubaliano hayo, kutokana na hatua ya Washington ya kuliwekea taifa hili vikwazo vipya.
-
Vikwazo vipya vya Marekani vinalenga kuzuia harakati ya kielimu na kiutafiti ya Iran
Jul 29, 2017 22:34Kama ilivyotarajiwa, Wizara ya Fedha ya Marekani imeyaweka mashirika sita ya Iran katika orodha yake ya vikwazo kama radiamali ya kukabiliana na jaribio la hivi karibuni la roketi la kubeba satalaiti la Simorgh hapa nchini.
-
SAUTI, Ripoti ya matukio ya Kiislamu kuanzia kilio cha Waislamu Kenya, Uganda na ongezeko la talaka za kiholela Zanzibar
Jul 29, 2017 10:54Ripoti ya matukio ya Kiislamu kuanzia malalamiko ya Waislamu kwa ofisi ya uhamiaji nchini Kenya ambayo inatajwa kufanya makusudi kuchelewesha kuwapatia pasi za kusafiria Waislamu zaidi ya 100 wanaotaka kwenda kushiriki ibada ya Hijja ya mwaka huu huo Saudia.
-
SAUTI, Tume ya Uchaguzi ya Rwanda yawaonya waangalizi wa uchaguzi wa ndani na nje kutoenda kinyume na kazi yao
Jul 29, 2017 10:47Tume ya uchaguzi nchini Rwanda imewaonya waangalizi wa uchaguzi kutoka ndani na nje ya nchi hiyo kutoingilia siasa za ndani za taifa hilo na badala yake wanatakiwa kuheshimu majukumu yao.
-
Syria yakosoa kuendelezwa vikwazo vya nchi za Magharibi dhidi yake
Jul 28, 2017 21:51Bashar Jaafari, Mwakilishi wa Kudumu wa Syria katika Umoja wa Mataifa amelaani mwendelezo wa vikwazo vya kidhalimu vya nchi za Magharibi dhidi yake na kusema kwamba vikwazo hivyo vimelemaza kabisa shughuli za mashirika ya misaada ya kibinadamu nchini humo.
-
SAUTI, Viongozi wa CUF Zanzibar wamekutana leo kujadili njia za kuchukua kufuatia hatua ya bunge dhidi ya chama hicho
Jul 28, 2017 12:20Viongozi wa chama cha wananchi CUF kutoka bara na visiwani nchini Tanzania wamekutana leo Zanzibar kujadili hatua ya hivi karibuni iliyochukuliwa na Spika wa Bunge la Tanzani Job Ndugai ya kuwapiga kalamu nyekundu wabunge wanane wa chama hicho kufuatia barua iliyowasilishwa na Profesa Ibrahim Haruna Lipumba, Mwnyekiti wa CUF anayetambuliwa na msajili wa vyama vya siasa nchini humo.
-
SAUTI, Waislamu nchini Kenya wakosoa vikali hatua ya Baraza la CIPK kujihusisha na siasa kwa kumpigia debe Rais Kenyatta
Jul 28, 2017 11:31Waumini wa dini ya Kiislamu nchini Kenya wamekosoa na kulaani kitendo cha Baraza la Maimamu na Wahubiri nchini Kenya CIPK kujitosa hadharani na kutangaza kumpigia debe Rais Uhuru Kenyetta wa nchi hiyo.
-
SAUTI, Magaidi wa Kikristo wa Anti-Balaka wanaendelea kuwazingira Waislamu ndani ya kanisa nchini CAR
Jul 28, 2017 11:30Magaidi wa kundi la Kikristo la Anti-Balaka wameendelea kuwazingira Waislamu wapatao 2000 waliokimbilia katika kanisa moj la mji wa Bangassou, yapata kilomita 700 mashariki mwa mji mkuu Bangui tangu tarehe 20 ya mwezi huu.
-
Wataalamu watangaza dawa ya kukinga Ukimwi, Mkutano wa Kimataifa wa Ukimwi, Paris
Jul 27, 2017 11:29Wataalamu walioshiriki katika Mkutano wa Kimataifa wa Ukimwi uliofanyika Paris nchini Ufaransa wametangaza mbinu mpya ya kuzuia maambukizi ya virusi vya HIV na kutibu maradhi ya Ukimwi.
-
Radiamali ya Wajordan dhidi ya jinai za ubalozi wa Israel na kimya cha serikali ya Amman
Jul 26, 2017 22:51Kuuliwa kwa kupigwa risasi raia wawili wa Jordan na mwanajeshi wa ubalozi wa Israel mjini Amman kumezua malalamiko na radiamali kali ya wabunge wa Jordan.