Magaidi wa ISIS waliokamtwa Iran wakiri kuhusu njama zao
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i10639-magaidi_wa_isis_waliokamtwa_iran_wakiri_kuhusu_njama_zao
Wizara ya Usalama ya Iran imetoa video ya magaidi wawili wa kundi la ISIS au Daesh ambao wamefafanua kuhusu njama zao za kupanga kutekeleza mashambulizi katika mji mkuu wa Iran, Tehran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 05, 2016 08:55 UTC
  • Magaidi wa ISIS waliokamtwa Iran wakiri kuhusu njama zao

Wizara ya Usalama ya Iran imetoa video ya magaidi wawili wa kundi la ISIS au Daesh ambao wamefafanua kuhusu njama zao za kupanga kutekeleza mashambulizi katika mji mkuu wa Iran, Tehran.

Katika mkanda huo wa video wa dakika 15 uliorushwa hewnai na Shirika la Utangazaji la Iran, IRIB, Jumatatu usiku, magaidi hao wa ISIS waliokamatwa hivi karibuni na vikosi vya usalama vya Iran wanaonekana wakieleza namna walivyopata mada za kutengeneza mabomu.

Aidha wanasema walilipwa Euro 600,000 kutekeleza mashambulizi ya mabomu katika maeneo 50 mjini Tehran na miji mingine mikubwa ya Iran.

Aidha wamebainisha namna walivyochukua muda wa wiki kadhaa kutafuta maeneo ya kutegea mabomu hasa maeneo yenye msongamano mkubwa wa watu.

Aidha mkanda huo wa video unaonyesha namna maafisa wa usalama walivyofuatilia kwa siri nyendo za magaidi hao huku wakirekodi kila hatua yao kabla ya kuwakamata. Hali kadhalika maafisa wa usalama walirekdi kwa video oparesheni yao maalumu ya kuwakamata magaidi hao.

Juni 20, Wizara ya Usalama ya Iran ilitoa taarifa kuhusu njama iliyofeli ya magaidi wakufurishaji kutekeleza hujuma za mabomu nchini katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.