Ugaidi hautambui mipaka
Katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia msururu wa vitendo vya uagidi ambavyo vimesababisha maafa na hasara kubwa tokea Lebanon hadi Iraq na Syria hadi Bangladesh.
Muda mfupi baada ya kutokea milipuko ya kigaidi Jumapili alfajiri huko Baghdad ambayo ilipelekea mamia ya watu kuuawa kinyama na wengine kujeruhiwa, milipuko mingine kama hiyo ya kigaidi ilitokea katika maeneo kadhaa huko Saudi Arabia siku ya Jumatatu alfajiri. Bahram Qassimi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alilaani vikali milipuko hiyo ambayo ilitokea karibu na Masjid an-Nabii na eneo la Qatif. Huku akiomboleza na familia za wahanga wa ugaidi huo, msemaji huyo wa Wizara ya Mambo ya Nje amesema kwamba kama ambavyo imekuwa ikifanya huko nyuma, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inalaani kila aina ya ugaidi popote pale unapokotokea na kutaka nchi zote zishirikiane katika kupambana na vyanzo, sababu na wahusika wa vitendo hivyo vya uagaidi.
Msemaji huyo wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran awali alikuwa amelaani pia ugaidi uliotekelezwa huko Bangladesh na kusema kuwa tukio hilo limethibitisha wazi kwamba ugaidi hautambui mipaka ya kijiografia, kitaifa wala kidini na kwamba njia pekee ya kupambana nao ni kuwepo ushirikiano wa nchi zote duniani.
Ugaidi ambao unashuhudiwa sasa katika eneo la Mashariki ya Kati uliikumba Iran miaka mingi iliyopita. Ugaidi huo bila shaka unatokana na siasa za kundumakuwili ambazo zinatekelezwa na nchi za Magharibi kupitia makundi mapya ya kigaidi kama vile al-Qaiada na Daesh. Kwa hakika Marekani inafunika uungaji mkono wake kwa ugaidi kupitia nara zake za hadaa eti za kupambana na ugaidi. Licha ya ugaidi kudhihirisha madhara yake kupitia matukio kama ya Septemba 11 2011 nchini Marekani lakini nchi hiyo inauarifisha ugaidi kwa vipimo vinavyolinda maslahi yake kwa kuugawa ugaidi katika makundi mawili ya ugaidi mbaya na mzuri na hivyo kutoyaweka baadhi ya makundi mashuhuri ya kigaidi katika orodha yake ya ugaidi na hivyo kuendelea kuunga mkono na kuyadhamini makundi hayo. Baadhi ya nchi za Kiarabu na kieneo kama vile Saudi Arabia na Uturuki zinayapa makundi ya kigaidi kila aina ya silaha za kisasa pamoja na fedha ambazo hutumika kuajiri vibaraka wa mataifa tofauti kwa ajili ya kuyahudumia makundi ya kigaidi yanayodhaminiwa na nchi hizo. Huo bila shaka ni uungajio mkono ugaidi.
Hivi sasa ambapo nchi za magharibi mwa Asia zimekumbwa na matatizo yanayotokana na kutokuwepo uthabiti wa kisiasa na mapambano dhidi ya ugaidi, madola yanayoingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine duniani yamevuruga zaidi hali ya eneo kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi huku yakiwatuhumu Waislamu kuwa ndio wanaohusika na ugaidi huo. Tarehe 29 Septemba mwaka uliopita, Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliwaandikia barua vijana wa nchi za Magaharibi akiyataja matukio ya kigaidi yaliyotokea nchini Ufaransa kuwa machungu. Awali mwezi Januari mwaka 2014 pia aliwatumia ujumbe muhimu vijana wa Ulaya na Amerika ya Kaskazini kuhusiana na chanzo cha ugaidi duniani. Katika barua zote mbili, Kiongozi Muadhamu aliashiria siasa za kundumakuwili za Wamagharibi na kusema kwamba wakati ambao watu wa Ulaya walikuwa wanasalia kwenye nyumba zao na kujiepusha kufika kwenye maeneo ya mikusanyiko ya umma familia za Wapalestina hazijasalimika hata kwenye nyumba zao zenyewe ambapo zimekuwa zikiishi kwa makumi ya miaka chini ya jinai na mauaji makubwa yanayotekelezwa dhidi yazo na utawala haramu wa Isreal. Mitazamo na misimamo ya wazi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inathibitisha wazi kwamba nchi hii imekuwa ikilichukulia suala la kupambana na ugaidi kuwa jambo la dharura kwa sababu hautambui mipaka yoyote ya kijiografia, kitaifa wala kidini na hivyo kutaka nchi zote zishirikiane kwa ajili ya kuutokomeza kabisa.