Feb 25, 2024 06:24 UTC
  • Kufufuka uhusiano wa Iran na Sudan kwaitia wahka mkubwa Marekani

John Godfrey, balozi wa Marekani nchini Sudan, amesema katika taarifa ya uingiliaji wa wazi wa mambo yasiyomuhusu ndewe wala sikio kwamba eti ana wasiwasi wa kuimarika uhusiano kati ya Iran na Sudan kwa madai kuwa uhusiano huo utaifanya Iran iisaidie kijeshi Sudan.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Fars, zaidi ya miezi minne imepita tangu nchi mbili za Iran na Sudan kutangaza kurejesha uhusiano wa kidiplomasia baina yao, hivi sasa Marekani na baadhi ya duru zinaingilia mara kwa mara uhusiano huo kwa visingizio mbalimbali.

Katika tukio la hivi karibuni kabisa, John Godfrey, balozi wa Marekani nchini Sudan amesema katika mahojiano na waandishi wa habari kwamba: "Kuna ripoti za kuwa, kurejeshwa uhusiano kati ya Iran na Sudan kunaweza kujumuisha uungaji mkono wa kijeshi wa Iran kwa Sudan. Hili ni jambo linalotutia wasiwasi."

Amedai kuwa nchi za kigeni hazipaswi kuzipa silaha pande zinazopigana huko Sudan, wakati Marekani yenyewe ndiye muuzaji mkubwa wa silaha duniani ikiwemo kwa makundi hasimu nchini Sudan.

Uhusiano wa Iran na nchi za Afrika unazitia kiwewe nchi za kibeberu na Kizayuni

 

Matamshi hayo ya kijuba ya balozi wa Marekani nchini Sudan yamekuja baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan, Ali al-Sadiq Ali kusema siku ya Jumatano iliyopita katika mkutano na mabalozi wa nchi hiyo kwamba kufufua uhusiano wa kidiplomasia na Iran ni jambo la kawaida na halina tatizo lolote.

Alisisitiza kuwa uhusiano huo si kwa madhara ya nchi yoyote ya tatu wala ya kikanda au kimataifa.

Tarehe 16 mwezi huu wa Februari, Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan alitembelea Iran na kukutana na kuzungumza na viongozi wa ngazi mbalimbali wa Jamhuri ya Kiislamu katika ziara rasmi ya hapa Tehran.

Hii ilikuwa ni ziara ya kwanza ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan kuitembelea Tehran baada ya kusitishwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili mwaka 2015. Kufuatia shambulio dhidi ya ubalozi wa Saudia mjini Tehran na ubalozi mdogo wa nchi hiyo mjini Mashhad yaliyottokea mwezi Januari 2014, Sudan iliungana na Saudi Arabia kukata uhusiano wao wa kidiplomasia na Iran lakini hivi sasa nchi hizo zote zimerejesha uhusiano wao na Jamhuri ya Kiislamu.

Tags