Jenerali Ghorbani: Vikwazo vimeimarisha mfumo wa kijeshi wa Iran
(last modified Thu, 15 Aug 2024 07:45:32 GMT )
Aug 15, 2024 07:45 UTC
  • Jenerali Ghorbani: Vikwazo vimeimarisha mfumo wa kijeshi wa Iran

Naibu Mratibu wa Kikosi cha Nchi Kavu cha Jeshi la Iran amesema kuwa vikwazo vya kikatili dhidi ya Iran havijakuwa na matokeo mengine ghairi ya kuimarisha mifumo ya kijeshi ya Jamhuri ya Kiislamu.

Brigedia Jenerali Yousef Ghorbani amesema kuwa, leo hii ushawishi, uwezo na mamlaka ya Iran ni ya kipekee duniani na kuongeza kuwa, "Licha ya vitisho vya maadui, tumezidi kuwa na nguvu zaidi siku baada ya siku katika miongo minne iliyopita na kusambaratisha nguvu ya madola ya kiistikbari."

"Miaka 45 ya vikwazo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeimarisha mifumo ya kijeshi ya Iran," Brigedia Jenerali Yousef Ghorbani amenukuliwa akisema hayo na shirika la habari la IRNA.

Ameeleza bayana kuwa: Licha ya ulinzi wa hali ya juu wa utawala wa Kizayuni, lakini tumeshuhudia operesheni madhubuti dhidi ya utawala huo katika Operesheni ya Ahadi ya Kweli.

Uwezo wa kijeshi wa Iran

Ikumbukwe kuwa, ubunifu na uamuzi wa Iran wa kumtia adabu mchokozi kwa operesheni ya Ahadi ya Kweli umetokomeza na kufuta uwezo hewa na bandia wa kuzuia hujuma na mashambulio wa utawala wa Kizayuni.

Naibu Mratibu wa Kikosi cha Ardhini cha Jeshi la Iran ameongeza kuwa, vikosi vya jeshi la Iran daima vinasimama upande wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Tags