China: Tunaunga mkono kuheshimiwa usalama wa kitaifa wa Iran
(last modified Sat, 02 Nov 2024 02:57:27 GMT )
Nov 02, 2024 02:57 UTC
  • China: Tunaunga mkono kuheshimiwa usalama wa kitaifa wa Iran

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya China imetangaza kuwa, inaunga mkono juhudi za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran za kudumisha uthabiti na usalama wake wa taifa  dhidi ya aina yoyote ya ugaidi.

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya China imetangaza kuwa, inaunga mkono juhudi za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran za kudumisha uthabiti na usalama wake wa taifa  dhidi ya aina yoyote ya ugaidi.

Hayo yameelezwa na msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa China Lin Jian katika mkutano na waandishi wa habari na kubainisha kwamba, "China inalaani mashambulizi ya kigaidi, inapinga aina zote za ugaidi, na inaunga mkono juhudi za Iran za kudumisha utulivu na usalama wake wa kitaifa."

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya China amesema kuwa, Beijing inapinga vikali hatua ya kukiukwa mamlaka ya kitaifa ya mataifa mengine.

Lin Jian amesema hayo akijibu hatua ya hivi karibuni ya kichokozi ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Iran na kusisitiza kwamba, China inapinga hatua yoyote ya kukiuka mamlaka ya kitaifa na usalama wa nchi nyingine na kutumia nguvu na mabavu mtawalia.

Vile vile amesema, baadhi ya matukio kwa mara nyingine tena yameonyesha udharura na ulazima wa kusitishwa mapigano na kuhitimisha vita.