Kiongozi Muadhamu ahudhuria hafla ya Qur'ani siku ya kwanza ya Ramadhani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i136828-kiongozi_muadhamu_ahudhuria_hafla_ya_qur'ani_siku_ya_kwanza_ya_ramadhani
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei amehudhuria kikao cha kiroho cha Qur'ani katika siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, akijumuika na maqarii na wasomaji mashuhuri wa Iran na kimataifa wa Qur'ani Tukufu.
(last modified 2026-02-20T03:28:20+00:00 )
Feb 20, 2026 03:28 UTC
  • Kiongozi Muadhamu ahudhuria hafla ya Qur'ani siku ya kwanza ya Ramadhani
    Kiongozi Muadhamu ahudhuria hafla ya Qur'ani siku ya kwanza ya Ramadhani

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei amehudhuria kikao cha kiroho cha Qur'ani katika siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, akijumuika na maqarii na wasomaji mashuhuri wa Iran na kimataifa wa Qur'ani Tukufu.

Mkusanyiko wa kila mwaka wa Ramadhani unaonyesha jukumu kuu la Quran Tukufu katika maisha ya kitamaduni na kiroho ya Jamhuri ya Kiislamu, huku ukiimarisha umoja na ibada ya kidini mwanzoni mwa mwezi huu mtukufu.

Hafla hiyo ilifanyika alasiri ya jana Alkhamisi katika Husseiniya ya Imam Khomeini mjini Tehran. Wasomaji mashuhuri wa Qur'ani wa Iran na kimataifa walisoma Aya za Quran Tukufu mbele ya Kiongozi.

Hafla hii inaashiria moja ya programu muhimu za kidini ambazo kwa kawaida hufanyika mwanzoni mwa Ramadhani nchini Iran.

Baada ya hafla ya kusoma Qur’an, Ayatullah Khamenei alitoa shukrani kwa "visomo vya hali ya juu na vizuri" wakati wa hafla hiyo.

Kiongozi Muadhamu aliwashukuru wasomaji na wanaharakati wa Qur'ani kwa juhudi zao za kutangaza mafundisho ya Qur'ani na kuimarisha maadili ya kiroho katika jamii.

Huusseiniya ya Imam Khomeini huandaa mara kwa mara matukio makubwa ya kidini na kitaifa yanayohudhuriwa na maafisa wakuu na wasomi.

Ratiba za Ramadhani kote Iran zinajumuisha vikao vya kusoma Quran, mipango ya hisani, na mikusanyiko ya iftar ya kijamii inayolenga kuimarisha mshikamano wa kijamii.