Military Watch: Ni vigumu kutungua makombora ya hypersoniki ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i137166-military_watch_ni_vigumu_kutungua_makombora_ya_hypersoniki_ya_iran
Jarida lenye sifa za kitaalamu la Military Watch limeripoti kuwa kombora jipya la Iran linalojulikana kwa jina la “Fatah-2”, ni changamoto kubwa kwa mifumo ya ulinzi ya Magharibi na waitifaki wake.
(last modified 2026-03-05T04:05:23+00:00 )
Mar 05, 2026 04:05 UTC
  • Military Watch: Ni vigumu kutungua makombora ya hypersoniki ya Iran

Jarida lenye sifa za kitaalamu la Military Watch limeripoti kuwa kombora jipya la Iran linalojulikana kwa jina la “Fatah-2”, ni changamoto kubwa kwa mifumo ya ulinzi ya Magharibi na waitifaki wake.

Jambo hili linalotokana na kasi yake ya ajabu na uwezo wake mkubwa wa kujizungusha na kubadilisha mwelekeo kwa urahisi, jambo ambalo linafanya kuwa vigumu sana au hata kutowezekana kulizuia na kulitungua.

Kulingana na taarifa za ISNA, jarida la uchambuzi wa Military Watch, baada ya kuchapisha picha za mashambulizi ya hivi karibuni ya Iran dhidi ya ngome za utawala wa Israel, limesema teknolojia iliyotumika katika kombora la Fatah-2 ni ya kizazi kipya na italeta mabadiliko kijeshi katika eneo.

Uchambuzi huu unasisitiza kuwa Iran imepunguza kwa kiasi kikubwa uwezo wa ulinzi wa Israel, kwa kujiunga na kundi la nchi zenye makombora ya hypersoniki (glider). Ripoti hiyo inaelezea kuwa kuingia kwa Iran katika kundi hili la teknolojia ya hali ya juu, linalowakilisha hatua kubwa ya mageuzi, na changamoto kubwa kwa mfumo wa ulinzi wa utawala wa Kizayuni wa Israel.