Iran yawakamata 'mamluki na majasusi' 36 wa Marekani, Israel
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i137396-iran_yawakamata_'mamluki_na_majasusi'_36_wa_marekani_israel
Jeshi la Polisi la Iran limefanikiwa kutambua na kuvunja mtandao wa mamluki na majasusi uliokuwa ukiongozwa na mashirika ya kijasusi ya Marekani na utawala haramu wa Israel ndani ya Iran.
(last modified 2026-03-16T05:18:59+00:00 )
Mar 16, 2026 05:18 UTC
  • Iran yawakamata 'mamluki na majasusi' 36 wa Marekani, Israel

Jeshi la Polisi la Iran limefanikiwa kutambua na kuvunja mtandao wa mamluki na majasusi uliokuwa ukiongozwa na mashirika ya kijasusi ya Marekani na utawala haramu wa Israel ndani ya Iran.

Polisi katika Mkoa wa Khuzestan, kusini magharibi mwa Iran imetangaza kuwa, imewatia mbaroni watu 36 wanaohusishwa na Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel, wakipanga kufanya hujuma dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.

Taarifa iliyotolewa na Polisi ya Khuzestan imeeleza kuwa, mamluki waliokamatwa walikuwa wanashirikiana na makundi yanayotaka kujitenga ya mkoa huo, wakipanga kuhujumu usalama wa taifa wa Iran wakati huu ambapo Marekani na utawala haramu wa Israel zinaendeleza mashambulizi ya kigaidi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.

Polisi ya Mkoa wa Khuzestan imeongeza kuwa, maafisa usalama wamenasa bunduki tatu na risasi 45 zilizokuwa mikononi mwa mamluki hao, ambao pia walikuwa wakipiga picha maeneo nyeti hapa nchini na kuwasambazia mabwana zao kwa ajili ya kuyashambulia.

Aidha imeelezwa kuwa, mamluki na majajusi hao wanaohusishwa na na Marekani na utawala wa Kizayuni walikuwa wanafanya mawasiliano na kanali inayosambaza propaganda chafu dhidi ya Iran ya 'Iran International'.

Habari zaidi zinasema kuwa, mtandao huo wa kuvuruga amani na usalama uliokuwa ukiongozwa na mashirika ya kijasusi ya Marekani na Israel ulitambuliwa ndani ya nchi na kusambaratishwa baada ya duru kadhaa za ufuatiliaji na hatua nyingine za kiintelijensia.

Si vibaya kukumbusha hapa kuwa, Januari mwaka huu, maafisa wa Iran walisema mamluki wa Marekani na Israel walihusika moja kwa moja katika machafuko yaliyoshuhudia hapa nchini wakati huo, ambapo watu zaidi ya 3,000 waliuawa shahidi.