Kamanda Mousavi: Iran sasa inadhibiti kikamilifu anga ya Israel
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i137518-kamanda_mousavi_iran_sasa_inadhibiti_kikamilifu_anga_ya_israel
Kamanda wa Kikosi cha Anga cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ametangaza kuwa makombora ya Iran sasa yanadhibiti kikamilifu anga ya utawala ghasibu wa Israel.
(last modified 2026-03-22T06:14:20+00:00 )
Mar 22, 2026 06:14 UTC
  • Kamanda Sayyid Majid Mousavi
    Kamanda Sayyid Majid Mousavi

Kamanda wa Kikosi cha Anga cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ametangaza kuwa makombora ya Iran sasa yanadhibiti kikamilifu anga ya utawala ghasibu wa Israel.

Kamanda Sayyid Majid Mousavi ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii kwamba: Mbinu na mifumo mipya ya kurushia makombora itakayoanza kutumika katika wimbi jipya la Operesheni Ahadi ya Kweli 4 itawaacha bumbuazi makamanda wa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kamanda Mousavi amesisitiza kuwa, usiku wa jana anga ya kusini mwa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Israel iliangaza kwa masaa kadhaa.

Matamshi haya ya Kamanda Mousavi yanaashiria mashambulizi makubwa yaliyofanywa jana usiku na vikosi vya majeshi ya Iran dhidi ya miji na maeneo kadhaa muhimu na ya kistratijia ya kusini mwa Israel ikiwa ni pamoja na shambulizi dhidi ya taasisi za nyuklia za Dimona ambapo Wazayuni zaidi ya 100 wanaripotiwa kuuawa na kujeruhiwa.